Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, January 25, 2011

UTARATIBU MPYA WA KUJISAJIRI KURUDIA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2011, JE WATOTO WA MASIKINI VIJIJINI WATAWEZA? soma hapa.

MAFUNZO YA UTARATIBU WA KUJISAJILI MTIHANI KWA KUTUMIA NJIA YA MTANDAO
Lengo la Kwanza: Utaratibu wa Kujisajili kwa Njia ya Mtandao

i. Mtahiniwa anatakiwa kujiandikisha kuwa mtumiaji wa huduma za mtandaoni za NECTA (NECTA Online Services).

ii. Kwa kufanya hivyo, mtahiniwa atapatiwa jina la utumiaji (user name) na nywila (password) ambavyo vitamwezesha kuingia katika huduma za mtandaoni za NECTA.

iii. Hatua kwa hatua, mtahiniwa atatakiwa kuingiza taarifa mbalimbali ili kukamilisha usajili wake.

iv. Mtahiniwa atatoa chapa ya fomu ya usajili (entry form).

v. Fomu ya usajili pamoja na ada ya mtihani husika itatakiwa kukabidhiwa kwenye ofisi ya posta ambako mtahiniwa atapewa risiti ya malipo.

vi. Posta watawasilisha fomu ya mtahiniwa NECTA pamoja na nakala ya risiti ya malipo ya ada. Posta watatakiwa kupiga muhuri kuthibitisha kupokea na kwamba malipo yamefanyika.

Lengo la Pili: Mahitaji Muhimu Kabla ya Kujiandikisha Kuwa Mtumiaji wa Huduma za Mtandaoni za NECTA

Ili mtahiniwa aweze kujisajili kwa njia ya mtandao anahitaji kuwa na mambo yafuatayo:

i. Ujuzi wa kompyuta wa kiwango cha kawaida cha mtumiaji. Ujuzi wa kutuma barua pepe unatosha kabisa kutumika kujisajili kwa njia ya mtandao. Kama mtahiniwa hana ujuzi wa kompyuta kabisa, basi, anaweza kuomba msaada wa mwenzake mwenye ujuzi wa kutosha.

ii. Awe na ufikio wa Intaneti. Ili kujisajili, mtahiniwa anatakiwa kuwa na ufikio wa Intaneti mara nyingi kwa kutembelea “Internet CafĂ©” yoyote au zile ambazo zimefunguliwa na Shirika la Posta.

iii. Mtahiniwa anaetaka kujisajili kwa njia ya mtandao ni lazima awe na anuani ya barua pepe ili aweze kujiandikisha kwenye mfumo wa usajili. Anuani ya barua pepe itatumika kumtumia mtahininiwa taarifa muhimu ikiwa ni pamoja na nywila mpya ikiwa ameisahau ya awali. Mtahiniwa pia anawezea kutumia anwani pepe ya mtu anaemuamini ikiwa yeye bado hajawa na anwani yake mwenyewe.

iv. Mtahiniwa anaetaka kujisajili kwa njia ya mtandao mtihani wa CSEE lazima awe yule ambae mtihani wake wa awali (QT au CSEE) alifanya kati ya mwaka 1988 hadi 2008. Kama mtahiniwa alifanya mitihani wake wa awali kabla ya 1988 ua alifanya mtihani wan je ya nchi, basi huyu atumie utaratibu wa zamani wa kujaza fomu zinazopatikana matawi yote ya posta.Lengo la Tatu: Kujua Faida za Kujisajili kwa Njia ya Mtandao

Baadhi ya faida ambazo mtahiniwa anaweza kuzipata iwapo atachagua kujisajili kwa njia ya mtandao ni pamoja na:

i. Mtahininiwa ataingiza taarifa zake yeye mwenyewe kwenye kompyuta. Hii inasaidia kupunguza makosa ambayo yangeweza kujitokeza wakati mtu mwingine (Mathalani ofisa wa NECTA) kuzikosea taarifa hizo wakati anaingiza kwenye kompyuta zetu.

ii. Mtahiniwa atapata fursa ya kujua mapema kama ana sifa au la. Hii inawezekana kwasababu kama mtahiniwa hana sifa mtandao utamjulisha pale pale na kama ana sifa pia atajua hapohapo. Kinachobaki ni kusubiri kutumiwa barua ya kumjulisha namba yake ya mtihani tu.

iii. Kwa kuwa mtahiniwa atakua na anwani pepe, basi taarifa nyingine zozote zinaweza kutumwa kwake mapema zaidi kuliko kusubiri barua rasmi ambayo inaweza kuchukua muda mrefu kidogo hadi kumfikia mtahiniwa.

Lengo la Nne: Kujiandikisha Kuwa Mtumiaji wa Huduma za NECTA Mtandaoni

Mtahiniwa anatakiwa kwanza kujiandikisha (kufungua akaunti) kwenye mfumo wa usajili (registration system). Uandikishaji huu ni muhimu ili mtahiniwa aweze kupata jina la utumiaji (user name) na nywila (password) vitu ambavyo vinahitajika ili mtahiniwa aweze kufikia mfumo wa usajili.

Mtahiniwa anatakiwa kufuata hatua zifuatazo ili aweze kujiandikisha:

Hatua ya Kwanza

Kwenye tovuti ya www.necta.go.tz, mtahinwa anatakiwa kubofya kiungo “private candidate registration”. Kiungo hicho kitampeleka kwenye ukurasa uonekanao kwenye picha Na. 1 hapo chini.Picha Na. 1

Mtahiniwa anatakiwa kubofya kiungo “Open Account” kinachoonekana kwenye Picha Na. 1 na kupata fomu ya kujiandikisha kama ionekanavyo kwenye picha Na. 2 hapo chini.

Picha Na. 2

Hatua ya Pili

Mtahiniwa anatakiwa kujaza fomu ionekanayo mchoro wa kurasa wa pili. Sehemu zote zenye alama ya * ni lazima zijazwe bila kuachwa wazi. Aidha mtahiniwa anatakiwa kubaini na kuingiza neno maalumu linaloonekana kwenye “Image Verification” ili kukamilisha zoezi la kujiandikisha.

Baada ya hapo mtahinwa anatakiwa kubofya kibonye ‘Register” ili kuwasilisha taarifa zilizojazwa kwenye fomu.Hatua ya Tatu

Baada ya kubofya kiungo “Register”, mtahiniwa atapelekwa kiotomati kwenye ukurasa wa kuingia kwenye mfumo.

Lengo la Tano: Kujisajili Mtihani wa CSEE

Hatua ya Kwanza

Katika picha na. 1, mtahiniwa atatakiwa kuingiza jina la utumiaji na nyila ili aingie kwenye mfumo wa usajli. Baada ya hapo mtahiniwa atabofya kiungo “Loging” ambacho kitampeleka kwenye picha na. 3 kama inavyo onekana hapo chini.Picha na. 3

Hatua ya Pili

Katika picha na. 3, mtahiniwa anatakiwa kuchagua njia atakayotakiwa kufanya malipo ya ada ya mtihani. Kwa kubofya kiungo “Posta Payment”, mtahiniwa atakua amechagua malipo kwa njia ya posta na hivyo atapelekwa kwenye picha na. 4.

Picha na. 4

Hatua ya Tatu

Katika hatua ya tatu, mtahiniwa anatakiwa kuchagua aina ya mtihani anaotakiwa kujisajili kati ya CSEE au QT.

Hatua ya Nne

Mtahiniwa akibofya kiuongo “New CSEE Registration” atapata picha na. tano kama unavyoonekana hapo chini.Picha na. 5Hatua ya Tano

Katika hatua hii mtahinwa anatakiwa:

i. Kuchagua mtihani unaompa sifa ya kufanya CSEE,

ii. Kuingiza namba ya mtihani huo,

iii. Kuchagua mwaka aliofanya mtihani huo.

Baada ya kuingiza taarifa hizo, mtahiniwa anatakiwa kubofya kibonye “Next”.

Hatua ya Sita

Kama mtahiniwa hana sifa, mfumo utamtaarifu katika hatua hii na hautampa fursa ya kuendelea na usajili. Vinginevyo, kama mtahiniwa ana sifa, mfumo utampeleka kwenye picha wa 6.Picha na. 6

Hatua ya Saba

Mtahiniwa mwenye sifa atapata fursa ya kujaza fomu inayoonekana kwenye picha na. 6. Baada ya kujaza fomu hiyo, mtahiniwa abofye kibonye “Next” ili apelekwe kwenye ukurasa uonekanao kwenye picha na. 7 kama inavyoonekana hapo chini.

Picha na. 7aPicha 7b

Hatua ya Nane

Hapa mtahiniwa ni lazima ajaze kwa kubofya tiki masomo yasiyozidi kumi katika picha na. 7a ambayo anataka kujisajili kufanya mtihani.

Kama mtahiniwa anatarajia kufanya masomo ya physics, chemistry au biology, masomo hayo yanachaguliwa kwenye picha namba 7b ili yaonyeshe na aina ya practical mtahiniwa anatarajia kufanya.

Baada ya hapo mtahiniwa anatakia kubofya kibonye “Register” kuendelea.Hatua ya Tisa

Mtahiniwa atapewa muhustasari wa taarifa zake za usajili katika picha na. 8 na kasha kutakiwa kuthibitisha au kughairi usajili wake.Picha na. 8

Mtahiniwa akibofya kiungo “Confirm Registration” usajili wake utawasiliwa na mtahinwa hataweza tena kufanya mabadiliko/marekebisho yoyote.

Aidha mtahiniwa akibofya kiungo “Cancel Registration”, mfumo utafuta taarifa zake zote alizojaza awali za usajili na utampa fursa ya kuanza tena upya kufanya usajili ulio sahihi.Hatua ya Kumi

Kwa mtahiniwa atakae bofya kiungo “Confirm Registration”, atapelekwa kwenye Picha na. 9 ambako atapata fursa ya kuchapa fomu yake ya usajili (entry form).Picha na. 9

Kwa kubofya kiungo “Print CSEE Entry Form”, mtahinwa ataweza kuzinza fomu yake ya usajili na kasha kuichapa.

Hatua ya Kumi na Moja

i. Fomu iliyochapwa inatakiwa kusainiwa na kupigwa mhuri na mkuu wa kituo mtahiniwa anachotegemea kufanyia mtihani.

ii. Fomu iliyochapwa pamoja na ada ya mtihani inatakiwa kuwasilishwa ofisi za posta ambako mtahiniwa atapatiwa risiti ya malipo ya ada.

iii. Posta watawasilisha fomu zote za usajli pamoja na nakala za risiti ya malipo kwa kila mtahiniwa alie wasilisha fomu zake posta.

Hadi hapa, usajili wa mtahiniwa anaetaka kufanya mtihani wa CSEE unakua umekamilika.Hatua za Usajili wa QT

Hatua ya Kwanza

Mtahiniwa anaetaka kujisajili kufanya mtihani wa QT, nae anatakiwa kufanya hatua zote tatu za kujiandikisha kama mtumiaji wa mfumo wa usajili. Hatua hizi zimeelezewa kwenye kurasa za mwanzo za andiko hili.

Hatua ya Pili

Kwa kutumia jina na nywila yake, mtahiniwa ataingia kwenye mfumo wa usajili ambapo atapata picha na.3 (taz. Ukurasa wa 3 wa andiko hili). Hapa mtahinwa atabofya kiungo “Posta Payment” ili apate picha na. 4.

Hatua ya Tatu

Kwenye picha na.4 mtahiniwa anatakiwa kubofya kiungo “New QT Registration” ili afikie picha na.10 kama inavyoonekana hapo chini.Picha na. 10Hatua ya Nne

Katika hatua hii mtahiniwa anatakiwa kujaza fomu juu ya taarifa zake binafsi pamoja na kituo anachotaka kufanya mtihani. Baada ya kuridhika, mtahiniwa atabofya kibonye “Register”.

Hatuta ya Tano

Mtahiniwa atapelekwa kwenye kurasa na. 11 ambako ataona muhustasari wa taarifa zake za usajili. Mtahinwa atatakiwa kubofya kiungo “Confirm Registration” kuthibitisha usajili wake au kubofya kiungo “Cancel Registration” kughairisha usajili wake.Picha na.11

Hatua ya Sita

Kwa watahiniwa watako thibitisha usajili wao watapelekwa kwenye picha na. 12 ili wachape fomu ya usajili (entry form) ikiwa na taarifa zote za usajili kwa kubofya kiungo “Print QT Entry Form”.

Picha na.12

Hatua ya Saba

i. Fomu iliyochapwa inatakiwa kusainiwa na kupigwa mhuri na mkuu wa kituo mtahiniwa anachotegemea kufanyia mtihani.

ii. Fomu iliyosainiwa ikabidhiwe ofisi ya posta pamoja na ada ya mtihani wa QT.

iii. Posta watapiga mhuri kwa kuthibitisha malipo ya ada yamefanyika na kisha kuwasilisha fomu zote pamoja na nakala ya risiti ya malipo NECTA.

Hadi hapa, usajili wa mtahiniwa anaetaka kufanya mtihani wa CSEE au QT unakua umekamilika.

Hitimisho

Hizo ndio hatua muhimu za kufuata ili kujisajili kufanya mtihani wa CSEE au QT. Afisa wa Posta anatakiwa kuwa makini na kuhakikisha hatua zote zinafuatwa kwa umakini.

Wahitimu wa mafunzo haya wanatakiwa kufanya mazoezi ya kutosha ya usajili kwa kutumia mtandao ili hatimae waweze kuwaelekeza na kutoa msaada wa kiufundi kwa watahiniwa watakotaka kujisajili kwa njia ya mtandao.

No comments: