Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, August 19, 2013

NDEGE YA TROPICAL YALETA UKOMBOZI MBEYA
Na Gordon Kalulunga, Mbeya

UNAFUU wa nauli ya ndege ya kampuni ya Tropical Air (Z) Ltd iliyoanza safari zake mkoani Mbeya takribani mwezi mmoja sasa, umekuwa mkombozi wa wananchi wanaopenda kusafiri kwa usafiri huo.

Baadhi ya abiria waliozungumza na Tanzania daima katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Songwe uliopo wilaya ya Mbeya Vijijini jana, walisema kuwa uwekezaji wa namna hiyo unaonesha tija kwa wananchi badala ya kuwakomoa.

‘’Ni ndege nzuri yenye nauli nafuu chini ya 200,000 tofauti na ndege zingine zinazofanya safari zake za Dar es Salaam na Mbeya’’ alisema abiria Antony Mavunde.

Tanzania daima, lilifika ofisi za ndege ya Tropical zilizopo uwanjani hapo na kukutana na meneja wa kampuni hiyo Ijaz Omar.

Meneja huyo alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikipata ongezeko la wateja siku hadi simu na ndege yao inao uwezo wa kupakia abiria zaidi ya arobaini.

‘’Bei zetu ni 180,000 kwa safari ya kwenda tu. Pia ndege yetu mbali na ukubwa wa kutosha ina hadhi’’ alisem Omar.

Alisema ndege hiyo, inafanya safari mara tatu kwa wiki ambapo ni siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na wanafanya mpango wa kupeleka huduma za usafiri katika mkoa wa Rukwa.

Kwa sasa kuna makampuni ya ndege mawili, yanayosafirisha abiria kupitia kiwanja cha Songwe ambapo baadhi nauli zao ni kuanzia 300,000 na kuendelea.

No comments: