Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, November 19, 2013

USAGAJI SASA BASI : NILIVYO INGIA NA KUTOKA KWENYE USAGAJI

Habari za leo wadau, baada ya kuwa busy kwa takribani miezi miwili sasa nimerudi kutimiza ahadi yangu, kama mnakumbuka siku kadhaa zilizopita niliahidi kuwa nitawaletea simulizi la maisha yangu ya usagaji jinsi nilivyo ingia kwenye usagaji, maisha yangu kwenye usagaji, athari nilizo zipata kwenye usagaji pamoja na jinsi nilivyo weza kutoka kwenye usagaji. 

 Ni matumaini yangu kuwa kisa cha maisha yangu kitasaidia kuielimisha jamii juu ya athari za usagaji.Fuatana na mimi hadi mwisho wa simulizi langu.
N.B : Kutokana na kuwa kwenye usagaji kwa muda mrefu sana nitakuwa nayaelezea matukio yangu kwa ufupi sana.


KWA MAONI AU USHAURI NIANDIKIE : konsolathathadeus@yahoo.com

SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ni mwaka 2001 nikiwa kidato cha tatu katika shule moja ya sekondari hapa jijini Dar Es salaam. Tulikuwa tunaishi Banana kipindi hicho. 


Jirani yetu kulikuwa na mdada mmoja ambaye by that she was like 27 or something. She was very generous na alikuwa ananisaidia mambo mengi tu kama vile hela, kuninunulia nguo nakadhalika. 

Mara kwa mara nilikuwa namtembelea nyumbani kwake na mara nyingi alikuwa anatembelewa na wageni wa kike wa umri tofauti tofauti, wageni wa kiume walikuwa ni kwa nadra sana kwake. 

Dada huyu alikuwa na ugomvi mkubwa sana na dada mwingine wa umri wake ambaye alikuwa amepanga jirani na alipokuwa anaishi huyo dada. 

Ilikuwa haipiti wiki bila kusikia hawa wadada wamegombana. Sikuwa najua sababu ni kitu gani zaidi nilihisi labda walikuwa wamenyan’ganyana mwanaume. 

Siku moja wakati natoka chumbani kwa huyu dada ambaye nitampa jina Mwajuma nilikutana na Yule mgomvi wake ambaye nitampa jina la Mwanne kwa sababu za kimaadili. Mwanne alipo niona akawa kama mtu aliye shtuka hivi. 

 Baadaye akaaniita pembeni na kuniambia kama namjua vizuri Mwajuma, nikamwambia yeah namjua vizuri ni kama dada yangu na amekuwa akinisaidia sana katika mambo yangu. 

Mwanne akaniambia,” Mwajuma si mtu mzuri sana kwako kuwa naye kwa makini sana, nilipotaka kuhoji zaidi akaniambia nijue hivyo hivyo, ila akaniambia iwe siri yangu nisimwambie chochote, nilibaki na maswali mengi sana kichwani, Mwajuma ni mtu mbaya kivipi? 

Ni mchawi anatoa watu kafara au anawauza mabinti kwa wanaume ? nilijiambia moyoni mwangu kama Mwajuma atakuwa ni mtu mbaya basi ubaya wake utakuwa ni kuwakuwadia wasichana kwa wanaume kwa sababu muda mwingi sana nimekuwa nikiwaona wasichana wakiingia na kutoka kwa Mwajuma so nikadhani labda itakuwa ndio tabia yake. 

Wiki tatu baadaye Mwanne aliniita chumbani kwake na kuniambia kuwa alikuwa ana hama usiku huo na kwa sababu alikuwa anahama usiku huo basi ataniambie kuhusu Mwajuma. Akaniambia kuwa
MWAJUMA NI MSAGAJI NA HATA CHANZO CHA UGOMVI WANGU NA YEYE NI KWA SABABU NILIMKATAA NA NINAHAMA HAPA KWA SABABU AMEKUWA AKINIFANYIA VITUKO VINGI NA KUNITISHA KUNITUMIA VIBAKA WANIFANYIZIE. Akaendelea kuniambia “ Mwanzoni Mwajuma alikuwa amenizoea kama alivyo kuzoea wewe, na alikuwa ananipa hela na vitu vyake kama anavyo kupa wewe, ila alikuwa ananikera kitu kimoja, ilikuwa kila siku lazima anipigie stori kuhusu wanawake wanao sagana, ilikuwa kila nikijaribu kubadilisha maongezi yeye anayarudisha kwenye usagaji na jinsi alivyokuwa anazungumzia usagaji alikuwa anaongea kwa hisia kali sana mpaka nikawa nasema huyu dada hayupo sawa sawa. Alikuwa kila akisoma gazeti lenye habari ya wasagaji basi huyo kiguu na njia atanifuata na kunionyesha halafu atataka siku nzima tuzungumzie usagaji tu na w asagaji. Siku moja nikiwa nyumbani kwake aliniambia kuna CD ameiona alipoiweka ilikuwa ni CD ya wanawake wasagaji wa kibongo wamejirekodi wakiwa wanasagana, nilipo muuliza hicho ni nini akaniambia ndio yale mambo aliyokuwa ananiambia ya wanawake kwa wanawake anaomba tuangalie wote, huku ananisogelea karibu yangu, nikamwambi a mimi siwezi kuangalia CD kama hiyo kwa sababu inanichefua roho, akanibembeleza sana nikagoma, nikwambia mimi sio mtu wa type hiyo na nikamwambia kama hana kitu kingine cha maana cha kuongea na mimi asiongee na mimi kabisa tena asinizoee, baada ya hapo nikaondoka kwa hasira coz aliniudhi sana niliona sijui huyu mwanamke amenionaje onaje. Basi kuanzia siku hiyo akawa adui yangu, kuna hela alikuwa amenipa akaniambia anaitaka, akaanza kuniomba nimpe vitu vyake vyote alivyo wahi kunipa and all that. Alinichukia sana na uadui kati yetu ukawa mkubwa sana ndo maana kila siku mkawa mnatuona tunagombana, kama hiyo haitoshi akaanza na kunitishia maisha mara ananitangazia kwa watu mimi mchawi na aliniambia nikimwambia mtu yoyote atanifanyia kitu kibaya, so angalia usije kuingia kwenye mtego wake “

Maneno ya Da Mwanne yaliniingia akilini barabara hasa nilipokuwa nikirudisha picha nyuma jinsi wasichana wanavyo pishana nyumbani kwa Da Mwajuma na jinsi alivyo kuwa mkarimu kwangu plus Mwajuma Alisha wahi kuniambia nisiwe naongea na Da Mwanne. 


Nilitafakari vitu vingi sana lakini hata hivyo badala ya kumchukia Da Mwanne nikajikuta Napata udadisi wa kutaka kujua inakuaje kuaje pindi mwanamke anapokuwa anasex na mwanamke mwenzake. 

Jioni ya siku hiyo Dada Mwanne akawa ameondoka nakumbuka ilikuwa siku ya Ijumaa, mimi nikapanga kwenda kumtembelea Dada MWAJU kesho yake na ikiwezekana nimuulize kuhusu nilicho ambiwa na Da Mwanne na kama inawezekana nione inakuwaje kuwaje. 

SOMO KUBWA HAPA : Kama unafahamu kuwa mwanamke Fulani mtaani kwenu anajihusisha na usagaji ni bora ukae kimya na usiwaambie watoto wa kike wakae naye mbali kwa sababu kati ya unao waambia miongoni mwao wapo wanao tafuta fursa ya kukutana na mwanamke wa aina hiyo, so be very careful.

Je Kitu gani kilitokea hiyo kesho yake? Kama mtapenda niendelee mseme na kama stori imewaboa nifahamisheni pia ili niachane nayo. ASANTENI SANA

Kwa maoni au ushauri nasaha tafadhali niandikie ; consolathathadeus@yahoo.com


chanzo;jamiiforum

No comments: