Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, March 29, 2014

ULIMWENGU USIOONEKANA


Wanabodi,
Huu ni muendelezo makala zangu kuhusu "works of powers", nguvu za kutenda miujiza, "psychic powers!", leo nitajikita zaidi katika nguvu za uponaji "faith healing!". Nitakuwa na maeneo yafuatayo.
1.    Faith Healing ni nini?.
2.    Faith Healing Inafanyikaje?.
3.    My Own Testimonial (ushuhuda wangu)
4.    Nguvu za Uponyaji zinatoka wapi?.
5.    Je Wahubiri wa Uponyaji ni Lazima wawe Wakristu?.

Nakuhakikishia, ni Hakika Asilimia 100% kwa 100% Uwezo huo unao, ila kwa vile hujitambui, hautumii!. Jitambue, utumie!.
1.    Somo la Kwanza, Faith Healing ni Nini?!.Kwa wale ambao ni wageni, nawashauri kabla hujaanza na uzi huu, wapitie kwanza hapa, Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila ...Na tuanze kwa kukumbushana tuu kidogo the basics!. Sisi binadamu tumeumbwa na Mungu kwa mfano wake. Ule uhai aliotupulizia, una nguvu za KiMungu ndani yetu!. Haijalishi wewe ni wa dini gani, ni wa imani gani, au hata wasio amini, wote tumeumbwa na Mungu, hivyo uwezo wa KiMungu uko ndani yetu, ni kwa kuutumia uwezo huu, ndipo muujiza hufanyika!.
2.    Faith Healing, ni uponyaji kwa kutumia imani!. Ambapo ule uponyaji huitwa muujiza. Hitoria ya kupona kwa miujiza ilianza zamani na sehemu kubwa ilijikita katika dini!, huko mimi siendi. Lengo la uzi huu ni kukujulisha wewe kuwa miujiza yoyote inayotokea, inawezekana kwa uwezo ilio ndani ya mtendewa muujiza na sio mtenda!.
3.    Hii Faith Healing ni kitendo cha mtu mwenye ugojwa fulani, kupona kwa njia ya imani tuu bila kutumia dawa yoyote, hivyo kipona kimiujiza, na uponyaji huu sometimes unahusisha hadi kukua wafu, au kuzui kifo, vipofu wanaona, visiwi wanasikia, bubu wanaongea, vilema wanaponyeka, viwete wanatembea, wagomba wanapata watoto, maradhi yoyote yanaponyeka.
4.    Miujiza hii imegawanyika katika makundi makuu matatu, ya kwanza ni ile miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe, muujiza mkuu ukiwa ni uumbaji! wa ulimwengu na kumuumba Adam. Miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe mingine ina sababu na mingine haina sababu, mfano muujiza wa kuiamuru bahari ya Sham kufunguka, ilikuwa na sababu ili Wana wa Israel wapite, lakini muujiza wa Bikiri Maria kupokea mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, haukuwa na sababu kwanini Maria, kulikuwa na mabikira wengi tuu!. Hii miujiza ya Mungu mwenyewe huitwa miujiza mikuu!. Miujiza iliofanywa na Yesu, nayo inaingia kwenye kundi hili la miujiza mikuu kufuatia imani kwa wanaomuamini Yesu ni Mwana wa Mungu, hivyo ni Mungu!
5.    Kisha kuna miujiza inayofanywa na sisi binadamu kupitia uwezo wa KiMungu ulio ndani yetu. Hii inajumuisha miujiza iliyofanywa na manabii, miujiza iliyofanywa na binadamu kwa uwezo wa Mungu ilio ndani yetu na mambo mazuri, na mema yote yanayofanyika duniani, ni kazi nzuri ya roho wa Mungu aliye ndani yetu.
6.    Pamoja na uwepo wa Mungu ndani yetu, mwovu shetani pia naye yupo duniani, na anazo nguvu kama za Mungu kutenda karibu kila kitu ambacho Mungu anatenda isipokuwa Mungu ana nguvu zaidi ya shetani!. jambo moja tuu!, upande wa uumbaji!. Yaani God is the creator and giver of life na ni ndani ya hii life ndimo zilimo nguvu za Mungu ndani yetu. Tofauti pekee kati ya Mungu na shetani, ni "life" shetani hawezi kuumba ila ndie muagamizi wa life. Maovu yote yanafanyika humu duniani ikiwemo miujiza ya uovu, ni kazi ya shetani. Zile sifa kuu tatu za Mungu, Omnipotence, hana mwisho, na shetani pia hana mwisho, tofauti ni Mungu ni wa milele na makao yake ya milele ni peponi, mbinguni au ahera kwenye furaha ya milele, na shetani makao yake ya milele ni motoni, kwenye ziwa la moto, akiungua na kuteseka milele!. Mungu ni Omnipresence, yaani yuko kila mahali, kitendo tuu cha mwanaadamu kupuliziwa pumzi ya uhai yenye Uuungu ndani yake, kunapelekea ndani ya kila binadamu kuna Mungu ndani yetu!, shetani naye alitupwa duniani, yeye na jeshi lake, nao pia wako kila mahali!. Mungu niOmniscience, ana uwezo wa kujua kila kitu kabla hakijatokea, there is nothing new under the sun, hivyo lolote litakalotokea, lilikuwa litokee, ila shetani naye ana uwezo wa kuijua mipango yote ya Mungu na kujitahidi kuiangamiza!.Hivyo faith healing ni uwezo wa kufanya miujiza ya uponyaji kwa kutibu kwa kutumia nguvu za Uungu zilizo ndani yetu, au kwa waliomkaribisha shetani ndani yao, basi ni uwezo wa iponyaji au kutibu kwa kutumia nguvu za shetani zilizo ndani yao!.

Somo la 2. Faith Healing unafanyikaje na inatibu vipi?.
1.    The most powerful thing kwenye mwili wa binaadami ni "will powers", "where there is a will, there is a way!. Hii "Will power" ni nguvu ya Mungu iliyo ndani yetu yenye uwezo wa kufanya kila kitu, ikiwemo miujiza!. Ili hii "will powers iweze kutenda miujiza, it has to be invoked!.
2.    Prescription ya faith healing, ni imani kuamini, na inafanyika kwa aina nyingi na kwa namna nyingi. Aina maarufu ni ile ya kuombewa na wahubiri/wachungaji/mitume/manabii/masheikh/viongozi wa dini/walokole/wanajimu/waganga wa kienyeji/watoa tiba mbadala etc, etc, dawa pekee kwenye tiba hii ni imani!. Kitendo cha kuamini ndicho kina invoke zile doors za forces of will to act upon a specific desease and cure it!.
3.    Kinachofanyika ni kwanza kutengeneza imani ya kuamini unachotakiwa kuamini. Kwa wale wa imani ya Kikiristu kwanza ni kuamini kwa dhati kuwa Yesu anakoa, Yesu anaponya, hivyo anayekuhubiria kwa kulitaja jina la Yesu, "Katika Jina la Yesu Zishindwe!", "Katika Jina la Bwana", etc, etc. Kitendo cha kuamini kuwa Yesu anaponya, kunafungua milango ya "powers of will" zilizo ndani yako ndizo zinazokuponya!. Kinachoponya ni nguvu ya Uungu iliyoko ndani yako, lile jina la Yesu, limetumika kama ufunguo tuu wa kufungulia hizo potentials zilizoko ndani yako!
4.    Wale wahubiri wa miujiza, wanachofanya ni kuutumia uwezo wao wa kuconvince ili kuifungua imani yako, ili ifungue hazina ya nguvu za uponyaji zilizoko ndani yako ndizo zinazotenda miujiza na sio yule mhubiri wala hilo jina!. Mhubiri ni make believe tuu na Jina la Yesu ndio ufunguo wa imani yako ili kufungua nguvu zilizo ndani yako kukuponya baada ya kuamini kwa dhati umepinywa!.
5.    Wako watu kibao wanatibu kwa faidh healing bila kulitaja jina lolote na watu wanapona!, kinachotakiwa ni kuamini tuu!, ndiko kunakofingua milango ya "powers" na haijalishi unaamini nini, iwe Mungu, Allah, Budha, Mti, jiwe, milima, kichuguu, hirizi, mganga or whoever, whataver as longo as unaamini utapona, unapona!.
6.    Namna ambayo hizo powers of will zinavyofanya kazi, ni un explainable scientifically, biologically, or medically, ila kinachoonekana ni matokeo tuu, viziwi wanasikia, vipofu wanaona, na viwete wanatembea na vilema wanaponyeka! ndio maana inaitwa miracles, miujiza na jina rasmi la kibinaadamu inaitwa ni kazi ya Mungu, au miujiza ya Mungu, na kwa vile nguvu zinazotumika ni nguvu za Mungu zilizo ndani yetu, hivyo ni haki kuita hii ni kazi ya Mungu.
7.    Wengi hukumbilia kwa wahubiri kuomba kuponywa wakati tayari wameathirika!. Kwa kujua kuwa hizo nguvu za uponyaji ziko ndani yetu, unaweza usisubiri hadi kuugua ndipo uinvoke will power ikutibu, ikiisha jitambua its you, and no one else, then unaweza kuivoke hiyo will powers ikazuia usipate ugojwa, yaani prevention is cure!.
8.    Hivyo kwa kuanzia anza kwa kujiandaa kuamini ili hiyo imani yako ifungue milango ya nguvu za Mungu za kufanya uponyaji zilizo ndani yak suo tuu zikuponye, bali pia kuzitumia as shield kuzuia magonjwa yoyote yasikufikie wewe na familia yako!.

Somo la 3: Ushuhuda Wangu (My Own Testimonials)
1.    Nikiwa primary, nilisumbuliwa sana na malaria, dawa zilikuwa choloquine, baadaya kupona nilikuwa nawashwa sana!, nikawa napewa na phenogan, lakini wapi, ukijumlisha nilikuwa kibonge na vipele vya jasho, ilikuwa baada ta kupona napata mateso makubwa zaidi kuliko hata nilivyokuwa naumwa!. Nikaanza kudevelop ioga wa dawa za malaria, hivyo nikiumwa, bora nisiseme, nijikaze hadi nikizidiwa saana ndipo niseme!.
2.    Thrugh nilipoingia sekondari uoga huu wa dawa,ukazidi, nikawa nikisikia dalili kwa mbali, napiga moyo konde, kisha dalili zinapotea. Tangu baada ya mulaliza sekondari, nilikaa 10 years bila kuugua malaria!. Mwaka 2000, nikapata trip ya Canada nikatakiwa kuomba migrant visa, inatolewa Nairobi, ila pia shurti upime ngoma kwenye accredited hosputal ilioorodheshwa, hivyo nikaenda Agha Khan hatua ya kwanza ni kupima full blood picture!, jamaa alinipima tuu, akaja ana shangaa, how could this man survive vidudu ving ajabu vya malaria sijui ni plus plis ngapi!.
3.    Jamaa wa maabara akaniita ni kuniambia nina malaria nyingi ya ajabu kiasi kwamba anashanga niko hai?. Kwa kiwango hicho, i was supposed to have been dead long ago!. Sikumuhadithia, nikamweleza hapa nimekuja kupima ngoma ndio mpango mzima!, jamaa akasema kwa kiwango cha malaria kilichopo, natakiwa kwanza kirudi kwa daktari, ndipo nikaridi kwa dakrati na vipimo, Dr pia akashangaa!. Akasema first thing natakiwa kuwa addmited haraka sana!, nikamgomea kuwa siumwi, sikubali kuwa addmited nahitaji tuu kipimo cha HIV!.
4.    Ndipo yule dr akanieleza kuwa huwezi kupimwa HIV kwa sababu damu yangi ina kiwango kikubwa mno cha vimelea wa malaria beyond human survival, hivyo white blood cells hazionekani kabisa!, kipimo cha ngoma enzi hizo kimbe kilikuwa kinapima tuu kiasi cha kinga iliyopio, wakikuta imeshuka, ndipo wanajua ni HIV+ve, akanieleza nina very chronic malaria, hivyo kipimo kitaonyesha ni positive hivyo ili nipime, ngoma lazima kwanza niitibu malaria!. Akanieleza hata wagonjwa wa TB wakiscreen inaonekana ni ngoma, ukiitibu ukapona ndipo inapimwa ngoma!.
5.    Hiyo daktari nikamweleza ukweli kuwa huwa naugua malaria lakini kutokana na kuogopa dawa, sithubutu kuitibu, its 10 years now!. Akashangaa na kusema hakuna hii kitu ya mtu kutougua malaria tropical Africa. Akanihimiza kukubali admission, pesa ikawa ni issue!, ndipo akaniambia kama tatizo langu lilikuwa chloroquine sasa kuna metakelfin na fansidar hivyo element ya kuwashwa hakuna!, lakini kutokana na kiwango kikubwa cha malaria kwenye damu yangu, ana recomend drip ya quinine ili kuipinguza kidogo kodogo!. Sina pesa za kulazwa Agha Khan, kwanza nimekwenda tuu hospitali hiyo kwa sababu ni mark hospital kwa migrant visa ya Canada.
6.    Hivyo nikasisitiza nipewe tuu vidonge. nikapewa metal kelfin kunywa winne siku ya kwanza, kisha vinne tena siku ya pili na viwili siku ya tatu, siku ya nne nirudi kucheki!. Siku hiyo nikanywa usiku, na maji mengi kwa maelekezo ya daktari!, mwili ulikuwa unawaka moto, sikulala usiku kucha ni kukoroma tuu kwa kugumia maumivu, kesho yake sikuweza kuamka, mwili wote umevimba, chakula hakipiti, maji hayapiti, siwezi kuamka, kiukweli nikajua sasa ndio safari!.
7.    By that time wife keshahamia US, na mimi naenda kuhamia Canada kwenye issue nyingine kama prospective husband wa a Tanzanian lady mwenye Canadian citizenship!. Hivyo nikaomba msaada home kwa wazee, nikafuatwa nikapelekwa Tumaini Hospital nikalazwa, wakachukua vipimo upya wakakuta kuvimba ni reaction ya sulfa, hivyo wakabadili dawa nitundikiwe drip ya quinine kuishusha hiyo malaria wakati huo mwili unajoto kali ajabu!.
8.    Drip ya kwanza imekwisha uvimbe umepungua lakini malaria bado ipo na homa bado juu, drpi ya pili ikaisha hsli ile ile, drop ya tatu naingia siku ya pili, hali ile ile, nikaona madaktari wanapisha, kama panic fulani, homa gani hii haishuki, Dr, Mkuu wa Pale Dr. Yongolo akasema ikifika siku ya tatu haijashuka, nitahamishiwa muhimbili!. Pia akamleta Dr Mmoja bnti mrembo toka Mhimbili akiita Dr. Masha Makata, Msukuma ni Msukuma tuu, hata mgonjwa vipi, binti mrembo mweupe!, mbona nilipata nafuu ghafla, nikakaa kitandani!.
9.    Kiukweli Masha alikuwa very friendly, akajaribisha dawa nyingine nyingine, homa ikashuka, vidudu vya malaria sasa havipo, lakini bado naumwa!. Nikaomba Masha aje baada ya ndugu kuondoka, ndipo nikaconfess kwake kuwa hii inawezekana kuwa ni ngoma!, nakamuomba akanipime kisiri siri ili nijue cha kufanya na sio kuunguza tuu fedha hospitalini. Akasema mgonjwa mwenye hali kama yangu, haruhusiwi kupima ngoma, ila kila mgonjwa anaelazwa kwa lolote, pia anapimwa ngoma, hivyo na wao walikuwa wanasubiri 7 days ndipo nipimwe!, nikaziona ni mbali, nikamsihi amisaidie, akanigomea kuwa yeye kama daktari hawezi, ila kunisaidia ataniitia mtu wa maabara niongee nae!.
10.                       Jamaa wa maabara akaja siku ya nne, akatoa damu, na kwenda kuipimia Mhumbili majibu atampa Masha. Siku hizo ukipima leo majibu kesho. Adubuhi ya suku ya 5, Dr. Masha kaja asubuhi, smiling na mimi nazidi kupata nafuu, huku riho inadunda. Niliisha panga nini cha kufanya iwapo nitakuwa positive maana nimeisha shuhudia shughuli ya kuwahudumia terminal ill HIV victims ndani ya familia, by the vidonge vya kupunguza makali vinatoka Nairobi au South na ku drain the family at the end of the day bado mtu ni safari!. Miliisha jiandaa kisaikolojia kuzuia kutesa watu!. Ndipo Masha akaniambia niko negative!. Amini usiamini nilipona pale pale nikataka kusimama drip ikanizuia!.
11.                       Mwaka huo wa 2000, ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kutibiwa malaria ndani ya miaka 10!, na ndio mara yangu ya mwisho kutibiwa malaria mpaka hii leo 14 years on, no more malaria!. Hata nikijisikia kuumwa, nikipimwa na kukutwa nayo, never again nitathubutu kuitibu!.

Somo la 4: Jee Nguvu Hizi za Uponyaji zinatoka wapi?.
1.    Msingi wa Nguvu za uponyaji ni Mungu, kwa jina lolote lile. Siku Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano ambapo mwili wetu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Mwili ni hii body inashikika, inaonekana, ina uzito, ina tabia zote za maada/matter. Sehemu ya pili roho, ni pale alipotuumba kwa ,fano wake na kutupulizia pumzi ya uzima, life, life force, spirit, spiritual body, astara body, roho, uhai. Kinachofanyika ndani yangu kuzuia malaria ni kufuatia ule uoga wangu kuogopa kuteseka na dawa za malaria, ninapo jisikia dalili tuu za awali kabisa, kwa mwili kuwa hypasensitive to touch, nikijigusa tuu vinyelea vya mkono, you feel something, then nasema kwa imani, it can't be malaria!. Hii inaitwa "denial the negativivity", kwa kujitamkia tuu maneno hayo kimoyo moyo, hiyo malaria stops there and then!.
2.    Hizo powers zipo ndani yetu zimehifadhiwa, namna ya kuzifungua ni kwa imani tuu!. Ukiamini, Milango ya powers inafunguka, "powers from within" zinaufanya mwili kuwa stronger na vile vidudu vya malaria harmless ila vipo!. Kadri siku zinavyokwenda vijidudu vinazidi ku pile, ila ni harmless. In ten years time vikawa vingi sana but harmless, nilipopimwa mpimaji anashtuka, daktari anashtuka, mimi niko ok.
3.    Kitendo cha kukubali kunywa ile dose, ni "accepting defeat" hivyo nika break ile barrier ya strenght ya powers from within, hivyo ile kinga ya mguva zangu ikatoweka, wale wadudu waliokuwa dormat wakarudi kuwa active, nisingewahiwa hospitali, pale ndio ingekuwa safari!. Once ukishajiaminisha kitu fulani kibaya kwako ni never, then don't and never accept defeat!. Ukiisha weka nia, never go back, ng'ang'ana hapo hapo hata kama hujaona matokeo spontaneously, never give up, Mungu ana namna zake za kujibu, halazimishwi!.
4.    Tangu ile 2000 mpaka leo, 2014, sijawahi kuugua tena malaria, lakini sasa sio mimi tuu bali na nyumba yangu yote, nimeishield, hatuugui malaria sisi wote tunaishi humo!. Nina watoto 7!, watano wakubwa na wawili wadogo. Wale wakubwa wote watano hawaishi home, wawili wakubwa wako chuo, mmoja yuko A level boarding na wawili wako O-level boarding, home niko na wale wadogo wawili tulio nao home malaria ni no tangu wamezaliwa ma hakuna trips za hospital zaidi ya cliniki. Wale wa boarding, sometimes wanapata malaria wakiwa shule/vyuo ila wakirudi home, no more malaria!.
5.    Baada ya kufanikiwa kwenye malaria, nikaamua kusema no kwa baadhi ya magojwa mengine!. Hata katika pita pita zangu, ukikutana na "njia" ambayo sio, machale yanakucheza hivyo sipiti "njia" hiyo!. Na baada ya kutopita, hautapita muda mrefu sana utasikia ya kusikia kuhusu ile "njia" uliotaka kupita!.
6.    Kwa vile hizi works of powers hazina uthibitisho wowote, scientifically, biologically, anatomically or medically to prove how they work, then siwezi kusema conclusive kwamba hizi kwangu ni powers za kuzuia malaria, inawezekana its just a game of chance kwamba mbumbu wote wanaingia nyumbani kwangu au kokote ni nilipo ni wale mbu wasio na malaria!.
7.    Pia licha ya kuwa na hiyo kinga dhidi ya malaria, au machale ya kuziepuka "njia" fulani fulani katika "pita pita" yangu, sasa badi ndio tusilale na neti, si tuna kinga?, au kule katika ile "pita pita" ndio nijipitie tuu peku peku ati kwa sababu nina kinga!. No way!.
8.    Hata wale wanaotibiwa maradhi kwa imani, haina maana akiumwa ndio asiende hospitali ati kwa sababu tuu anamtegemea Mungu!, au alikuwa na ukimwi, kifua kikuu, canser, akatibiwa kwa imani, akapona, basi hospitali ndio basi!, no!. Faith healing is not a substitute to medical treatment, but rather a complementary!.
9.    Namalizia kwa msisitizo, kuponywa kwa miujiza, nguvu za uponyaji zinatoka kwako wewe mgojwa mwenyewe na sio hiyo anayekuombea!. Wachungaji wengi au waganga, hujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za kuponya!, No way, wao wanakupatia tuu ufunguo wa kuzifungulia hizo nguvu zilizo ndani yako ndizo zinazoponya. Hata kile kikombe cha Babu, what you drink is nothing!, imani kuwa kikombe kinaponya ndio imewafungulia njia wenye imani, nguvu zao zilifunguka zikawaponya, na wale wenye imani haba, it was a waste, wastage of time and resources!.
10.                       Ukiwa na very strong faith kuwa sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo tunazo nguvu za Mungu ndani yetu, chochote utakachopanga kwa imani, kitafanikiwa!, sky is the limit!.

Anza sasa kuzifungua hizo nguvu zako na kuanza kuzitumia kufanya mambo madogo madogo.
Somo la 5: Je Wenye kuweza Kuponya wa Miujiza lazima wawe Wakristo?!.
1.    Baada ya kwanza kukubaliana kuwa Muumbaji wa Vitu vyote ni Mmoja, God!, The Creator!, haijalishi mtu una imani gani, au hata kama huna imani, maadam uliumbwa na Mungu na Mungu ndiye aliyeziweka hizi nguvu kwa viumbe wake, hivyo mbele ya Mungu, binadamu wote ni sawa, na wote wanazo hizi nguvu, na wote wanaweza kuzitumia na wamekuwa wakizitumia!.
2.    Kufuatia msimamo huu, watu wote wana uwezo wa kuponya na sii lazima wawe ni Wakristu ila kasi ya uponyaji kwa kutumia imani, imekuwa more popular na Wakristu kwa sababu wanaamini mwenye hizi nguvu za uponyaji ni kupitia kwa Jina la Yesu Pekee!. Ukweli ni kuwa, nguvu za uponyaji, ziko ndani yetu!, Ili uweze kuzitumia ni lazima kwanza uzifungulia milango "open the gates" hizi nguvu zilizofungiwa ndani yako, ndipo ziweze kufanya uponyaji, kitendo cha kuamini "Ni Katika Jina la Yesu!", hiyo ni catalyst tuu ya kuzifungulia milango!. Watu wengine wowote, wenye imani nyingine yoyote, pia wanaweza kuyafanya haya yote alimradi wazifungulie milango hizi nguvu kwa imani yoyote!.
3.    Wakristu wanaamini kawa muujiza wa kwanza wa uponyaji ulifanywa na Yesu, alipomfufua Lazaro, na kaendelea kuponya wagonjwa kwa vipofu kuona, viziwi kusikia, na wenye ulemavu mbalimbali kutakaswa, hivyo powers hizi za uponyaji zimehusishwa na Jina La Yesu, ndani ya Ukristo kama kulivyo na madhehebu mengi tofauti na yote yakimwamini Yesu, vivyo hivyo imani hii ya uponaji inatofautiana sana kati ya dhehebu na dhehebu, ambao Kanisa Katoliki liko makini sana na tiba hizi za imani, wakati makanisa ya wokovu, wakizikumbatia powers hizi kama fimbo ya kukamatia waumini na wafuasi.
4.    Kanisa Katoliki linaamini Mungu hufanya uponyaji pale tuu anapoamua kupitia nguvu alizowapa Makasisi wake ndani ya sala, hivyo hakuna utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa au wenye matatizo makanisani kuombewa, kwa sababu maisha yetu sii ya dunia hii, kinachotakiwa kufanyika kwa mgonjwa mahututi, ni kumpatia sakrament ya Upako Mtakatifu ili kumuondolea dhambi zake zote hapa duniani ili akifa aingie mbinguni au peponi moja kwa moja!. Na Baada ya kuzuka kwa wimbi kubwa la uponyaji, Askofu Milingo wa Zambia alitumia powers za asili kuponya makanisani, aliitwa na kupewa kifungo huko Vatican, na kwa hapa kwetu Tanzania, Pasdri Nkera nae alitimuliwa na kikundi chake cha Wanamaombi kikapigwa marufuku, lakini kufuatia wimbi kubwa la kupoteza waumini wanaokimbilia makanisa ya Wokovu, hatimaye Kanisa Katoliki limegeza masharti kwa kuwaruhusu watu wanaoitwa Wana Karismatiki kuendesha maombi ya uponyaji bali sio ndani ya nyumba za ibada!.
5.    Kwa vile tumetawaliwa zaidi na dini kuu mbili Ukristo na Uislamu, na hizi sio dini zetu za asili, nguvu za uponyaji wa miujiza zilikuwepo tangu zamani, enzi za mababu zetu, na wazungu na Waarabu walipokuja kutuletea dini zao, walitukuta na uwezo mkubwa, ila wakatuhadaa kuwa hao miungu wa asili tunaowaabudu, sio Mungu wa kweli, bali Mungu wa kweli ni Mungu wao God na Allah, hivyo wengi wetu kujikuta tumezaliwa kwenye hizi mbili kuu bila choice na wote huishia kujikita katika imani ya dini uliyozaliwa nayo tuu, lakini ukweli wa nguvu za uponyaji zaidi ya kwenye Ukristu, pia kwenye Uislamu upo, kwenye Hindu upo, kwenye Budhiism upo kila mahali na hata wengi waganga wa kienyewe, wale ambao ni waganga wa ukweli, ukiachana na hawa wa longo longo, nao wanazitumia nguvu hizi hizi za uponyaji zilizomo ndani yetu, ile kupiga manyanga ndio catalysti yenyewe ya kuzufungulia nguvu hizi za uponyaji zilizo ndani yako, ndizo zinazokuponya bila wewe kujijua huku ukiamini ni huyo Mganga!.
6.    Nguvu hizi za uponyaji, zinasemekana kuweza kuponya magonjwa yoyote yaliyoshindikanika mahospitalini ikiwemo AIDS, cancer, ugumba, vipofu kuona, vilema kutembea, viziwi kusikia, etc etc ila mimi kama mhanga wa ajali, nimefuatilia kwa karibu baadhi ya hawa wahubiri wanaojifanya wana uwezo wa uponyaji, sijaweza kufanikiwa kuuthibitisha uwezo huo!, nyingi na hivi mnavyoviona kwenye TV kama ni uponyaji, asilimia kubwa ni viini macho tuu, ila pia uponyaji wa ukweli upo kwa sababu unatokea ndani ya yule mgonjwa mwenyewe, ambaye anaponywa kwa imani yake huku mhubiri akichukua credts.
7.    Wengi wa hawa wahubiri wa makanisa ya Wokovu, wameishajua powers za uponyaji ziko ndani ya kila mtu, hiyo wanaihifadhi kama siri yao ila wanaitumia imani yako kukuponya and in return kuvuta fungu kwa hoja ya kufanya kazi ya Bwana, na mengi ya magonjwa yanayoombewa ni yale yasiyoonekana!, mapepo, magonjwa na ndani etc, sijapata kushuhudia popote hapa Tanzania kipofu anaona, kiziwi anasikia, kilema miguu inanyooka anatembea!, wengi wa hao mnaowaona kwenye TV ni stage acting to make believe!, ndio maana utaishia kuwaonea pale majukwaani tuu!, hakuna any follow-up ya uthibitisho wa ndugu, jamaa au majirani kuthibitisha huyu alikwa kilema sasa anatembea zaidi zile shuhuda za madhabahuni!,
8.    Kwa vile nguvu hizi za uponyaji ni za kutoka kwa Mungu, process nzima ya uponyaji bado haina scietific proof ya ni nini haswa kinatokea, mtu amekuwa dioginazed with aids then anaombewa, anarudi kupimwa, aids haipo tena!, kufuatia kukosekana kwa uthibitisho wa kidaktari ugonjwa huo umeponaje!, nasisitiza mtu ukiwa unaumwa chochote serious, pamoja na posibilitiy ya kujitibia kwa imani, nenda hospitalini ukapate ushauri wa kitabibu na sio kuzitegemea nguvu hizo pekee!. Kuna wengi walioitegemea imani pekee, wakaishia kupata maafa ya kufiwa, kufiliwa na kuwapoteza wapenzi wao, kwa magonjwa ya kawaida tuu ambayo mahositalini wangetibiwa na kupona!.

9.    Pamoja na kuwepo kwa uwezo huu wa uponyaji miongoni mwetu, pia sometimes utapeli wa iaina fulani pia upo!, utakuta wahubiri wetu hawa hawa, wanapofanya zaira za mahubiri nje ya vituo vyao vya kawaida, ndiko wanakofanya miujiza mikubwa ya ajabu!. Tumewashuhudia wahubiri wetu wakipokelewa na kukaribishwa Ikulu za watu wengi huko huko wakifanya uponyaji wa ajabu ambao hapa nyumbani hawaufanyi!, hizi ni make belive tuu na mwisho wa siku kitu muhimu kwao ni ile number ya M=Pesa/Airtel Money/Tigo Pesa au Z-Pesa ndio mpango mzima!.

10.                       Na mwisho kama nilivyoeleza kwenye mada zangu zilizotangulia, Mungu yupo ni mwenye nguvu na ndiye aliyetupatia huu uwezo ndani yetu!, ila pia shetani naye yupo!, na yeye pia ana uwezo!. Yesu alipoondoka alituasa kuwa "Watakuja watu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!", hivyo wale wenye imani haba, wanaweza kujikuta wanapotezwa maboya na hawa wahubiri wa miujiza wakidhani uwezo wao unatoka kwa Mungu, kumbe unatoka kwa shetani, na nguvu wanazotumia ni nguvu za giza!. Hivyo kuna uponyaji unafanyika kwa nguvu za Mungu na mwingine ni kwa nguvu za giza!.Jee utajuaje kama hizi ni nguvu za Mungu au ni nguvu za giza?!. The ony way kutambua ni kwa ku "listen from yourself!", " only the voice from wthin ndio inaweza kukuonyesha kweli!.

Nasisitiza hizi mada ni kwa watu ambao ni open minded!, Nawaomba sana wale wahafidhina na ma conservatives wa imani za dini zao, shikilieni mafundisho ya dini zenu, na wenye nia ya kuanzisha malumbano ya dini, tukutanie Jukwaa la Dini, tuwekane sawa!.

Natanguliza Shukrani.

SOURCE :  JAMII  FORUMS

No comments: