Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, April 24, 2014

ADNAN JANUZAJ KUCHEZEA NCHI YA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA

 
Winga wa Manchester United Adnan Januzaj amechagua kuiwakilisha timu ya taifa ya Ubelgiji katika mashindano ya kimataifa.
Kocha wa Ubelgiji Marc Wilmots ametoa tangazo kwenye ukurasa wa Twitter  na kusema "amefurahishwa" na uamuzi wa mchezaji huyo kinda.
 
Januzaj alizaliwa katika mji wa Brussels ambao ni mji mkuu wa Ubelgiji kwa wazazi wake wenye mchanganyiko wa Kosovo na Albania na alijiunga na United mwaka 2011.
 
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 angeweza kuzichezea nchi za Kosovo, Albania, Turkey, Serbia na England, lakini sasa ameitaja Ubelgiji kuwa ndiyo ataiwakilisha kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Dunia ambapo kikosi kamili cha wachezaji 30 kinatarajiwa kutajwa 13 May mwaka huu.
 
Alisaini United akitokea Anderlecht kwa ada iliyoripotiwa kuwa paundi 297,000, Januzaj angaliweza kuichezea timu ya taifa ya England kuanzia mwaka 2018 kama angaliendelea kubaki nchini humo kwa sababu sheria za Fifa zinaeleza kuwa mchezaji anaruhusiwa kuichezea timu ya taifa fulani endapo ameishi nchi humo kwa miaka mitano mfululizo tangu alipotimiza umri wa miaka 18.
 
Januzaj anaweza kuichezea timu ya taifa ya Albania kwa sababu ya wazazi wake na Uturuki kwa sababu ya babu na bibi yake. Pia angaliweza kuiwakilisha Serbia baada ya Kosovo kutangaza uhuru kutoka Serbia mwaka 2008.
 
Kufuatia mchezaji huyo kufanya vizuri kwenye klabu yake, Wilmots amesema alimhitaji kuichezea Ubelgiji, wakati meneja wa England Roy Hodgson akieleza kuwa alikuwa anamtupia jicho mchezaji huyo ambaye ametaja kuwa "mwenye kipaji".

No comments: