Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, April 24, 2014

MATERNAL NEWBORN AND HEALTH(MHN).

KUWA KINARA WA KUWAOKOA AKINAMAMA NA WATOTO WACHANGA

By, Gordon Kalulunga.

We could save up to 8500 Mothres who currently die each year.

Two thirds aof all newborn deaths Globally occur in 10 countries, Tanzania is one of them.

There is the possibility of saving the lives of up to 130 newborns every day.

Inasikitisha sana kwamba kila mwaka akinamama 8,500 wa Tanzania hufariki wakati wa ujauzito au kwa matatizo ya uzazi kila mwaka. Hali hii haikubaliki.

Maelfu ya kinamama hawa wangeokolewa kama wajawazito wote nchini wangekuwa na taarifa kuhusu dalili za hatari za ujauzito.

Wangejifungulia kwenye vituo vya huduma za Afya. Wangepata huduma ya kitaalam mara tu baada ya kujifungua.

Wanawake wote wa Tanzania, wanastahili kuvuka salama kipindi cha ujauzito na kujifungua. Ni kipindi cha kueta uhai wa binadamu duniani.

Wanawake wanapaswa kujifungulia katika vituo vya Afya lakini kituo hicho kinatakiwa kitoe huduma zifuatazo kwa wanawake wajawazito na waliojifungua.

Huduma ya kitaalamu, huduma bure ikiwemo dawa, huduma yenye kuzingatia utu. Mama zetu wanastahili kustahiwa na kuheshimiwa na kupata huduma sahihi kwa wakati hasa kwenye dharura. Hawapaswi kutukanwa wala kukajeliwa.

Sote ni muhimu kuhakikisha kituo cha huduma za Afya kilicho karibu kinatoa huduma hizi kwa sababu uhai wa mama na mtoto mchanga ni kipaumbele cha Taifa. 

Na kama kituo hakina huduma hizo basi ongea na diwani wenu, serikali ya kijiji au kata, au mkuu wa  kituo hicho.

Hata wewe unaweza kuleta mabadiliko;
Wahimize wanawake kujifungulia kwenye vituo vya huduma za afya na si majumbani.

Jenga matumaini-wafahamishe wanawake na wenza wao juu ya huduma wanazostahili kupewa kutoka kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu.

Hamasisha maandalizi ya kumwezesha mama mjamzito kujifungulia katika kituo cha huduma za afya kama vile usafiri, msindikizaji, chakula n.k

Kuwa mwanaharakati kuhamasisha uwepo wa Mfuko wa Afya ya Jamii kwenye kituo chenu ambao utahakikisha dawa na vifaa vingine muhimu vinapatikana bure kwa wajawazito kabla na baada ya kujifungua.

Wito wangu kwa jamii ya watanzania, kuchukua hatua kwa ajili ya akina Mama na watoto wachanga na kutokubali dhana potofu kuwa kifo wakati wa kujifungua ni jambo la kawaida au ni mipango ya Mungu.


Gordon Kalulunga
Information and Media Consultant
P.O. Box 705, Mbeya-Tanzania
Cell: 255 (0)754 440 749/255 (0)787 552 955
e-mail: kalulunga2006@gmail.com
www.kalulunga.blogspot.com

No comments: