Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, April 03, 2014

MBARONI KWA KUKUTWA NA KIDOLE CHA BINADAMU-IRINGA,


NA FRANK KIBIKI, IRINGA
 
WAKAZI wa kijiji cha Mazombe, mkoani Iringa wanashukiliwa na jesho la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na kidole cha binadamu kutokana na imani za kishirikina.
 
Kaim Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo limetokea juzi na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Gibson Kasenegala (29) na Benson Mlasu (23).
 
Alisema watuhumiwa hao, wakiwa pamoja walikuwa wakimiliki koidole hicho ambacho hakijulikanani cha nani, kutokana na imani za kishirikina kwamba kinaweza kuwasaidia kupata mali.
 
“Tumewatia mbaroni na uchunguzi wetu unaendelea ili tujue nani alikatwa kidole, au kama kuna mtu aliuawa kisha kidole chake kikachukuliwa,” alisema Nyigesa.
 
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi huo kukamilika.

No comments: