Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, April 04, 2014

SAUTI KUTOKA NYIKANI.....WARIOBA AMEVIZIWA KWENYE KONAMTEGO wa kuvizia mbaya. Adui huvizia wapinzani wake wanapopita katika eneo finyu, darajani, tindiga na kisha hufanya shambulio.

Pia mpinzani wako kisiasa anapogeuka ghafla kuwa rafiki yako, chukua tahadhali, unaweza kuwa mtego wa kuvizia. Hiki ndichoMzee Joseph Sinde Warioba hakukijua alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rasimu ya Mabadiliko ya katiba.

Jaji mstaafu Warioba alikubali uteuzi ule akidhani tofauti za kimsimamo kuhusiana na vita vya urais ndani ya CCM mwaka 2005 pale Jakaya Mrisho Kikwete alipopitishwa na kupeta tena mwaka 2010. Lakini hakujua kuwa mapambano ya kisiasa hayakumalizika.

Ndiyo, wakubwa wanaweza kupita kila mahala kuomba makundi yavunjwe, lakini wao hubaki na fundo moyoni. Hicho ndicho kimemtokea Jaji Warioba sasa anashambuliwa binafsi na siyo Tume aliyoiongoza.

Warioba hakuwa Tume, bali aliongoza watu 30 wakiwemo wanasiasa, mahakimu, wanadiplomasia na wasomi wa sheria waliobobea. Jiulize hao hawajui uzuri au ubaya wa Muungano wa serikali mbili?

Kati ya mwaka 1985 na 1990, Warioba alikuwa waziri Mkuu, mwaka 1995 aliwania urais pamoja na Kikwete lakini Benjamin Mkapa akashinda.

Mwanadiplomasia Dr. Salim, aliwania urais mwaka 2005 lakini akachafuliwa akidaiwa si raia.

Tuache hay. Warioba aliongoza Tume iliyosheheni wana CCM ambao kutoka Bara walikuwa Richard Lyimo, Alhaji Said El-Maamry, Prof, Kabudi, Humfrey Polepole, Yahya Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Kashonda, Aly Shyma J. kwegyir(MB), Mwantumu Malale na Joseph Butiku.

Wajumbe ambao hawakuwa wana CCM walikuwa Prof. Mwesiga Baregu, Riziki Mngwali, Dr. Sengondo Mvungi, John Nkolo, Jesca Sydney Mkuchu na labda Jaji Mtaafu Augustino Ramadhani.

Wana CCM kutoka Zanzibar walikuwa Dr. Salm, Fatma Said Ali, Omary Sheha Mussa, Simai Mohammed Said, Mohamed Yusuph Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omary Ali, Salama Kombo Ahmed, Abubakar Mohamed Ali.

Wasio wana CCM walikuwa Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Said, Ussu Khamis Haji, Salma Maoulid, Nasssor Hamiss Mohamed na Ally Abdullah Ally Salehe.

Makada hao wamekosea wapi hadi Warioba ashambuliwe kama mwanasesere? Je, kuna aliyewasaliti kwa kuvujisha siri namna walivyofikia maamuzi ya Serikali Tatu?

Kuna nini nyuma ya shutuma hizi? Je, Tume ya Warioba ilikuwa ya kutetea sera za CCM au kukusanya maoni na kuandaa rasimu ya Katiba mpya?

Sasa CCM imeibua shutma mpya, inasema Warioba amechakachua maoni.

Katika mkutano wa hadhara wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam wiki iliyopita, Katibu Mukuu, Abdulrahman Kinana, alidai, Warioba ameacha maoni ya mabaraza 200 yenye wajumbe wengi wa CCM akajikita kwenye mabadara matatu tu.

Hizi ni shutuma nzito.

Wariob ameviziwa, anashambuliwa kwasababu ya msimamo wake kuelekea uteuzi wa mgombea urais mwaka 2005.

Mtandao ulimbeba Kikwete, akawabwaga pamoja na wagombea wengine, Dr. Salmin aliyekuwa akiungwa mkono na akina Warioba na Butiku.

Rais Kikwete, hali akijua msimamo wa makada hawa, akawaweka katika Tume na sasa amepata sababu ya kuwananga ndani nan je ya CCM.  Wana CCM wengine wanapiga ngoma wasiyoijua.

Wewe fikiria, Tume hii ilikuwa inawasiliana  na Rais Kikwete kila hatua, kila mara ikitaka kujua msimamo wake, lakini hakutoa. Kwa nini hakuonesha msimamo? Alisubiri muda na fursa ya kuwadhalilisha peupeeeeeeeee.

JOSTER MWANGULUMBI
Credit;MAWIO

No comments: