Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, May 06, 2014

SAUTI YA NYIKANI....CHADEMA MBEYA WANAKUNYWA SUMU KISA WAMEONA MAZIWA!NA GORDON KALULUNGA

KWANZA nianze kwa kusema nitaunga mkono serikali tatu za UKAWA endapo Jusa, Rais Mstaafu wa Zanzibar Abeid Karume na Maalim Seif  Sharif Ahmad wakisema mipango yao ya sirini na nikipewa ufafanuzi na serikali hatua zilizochukuliwa baada ya uchomwaji wa Makanisa na ilikoishia mikakati ya kuitaka OIC.

Ukawa itavimaliza vyama vya siasa. Mnara wa baberi utatokea katikati ya wanaouunda umoja huo, kwasababu kila mmoja anajua anachokitafuta. Watagombaniana kijiti.

Wakati UKAWA ikiendelea, nimuombe Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, atupie jicho lake mkoani Mbeya, maana chama kinakwisha.  Sina huruma na Chadema, bali nina huruma na demokrasia.

Hivi karibuni, katika  chama hicho wilaya ya Mbeya Mjini, kumeibua mambo ambayo siyo mapya kwa chama hicho.

Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho pia Mkufunzi wa mafunzo ya Redbriged kanda ya Nyanda za juu kusini,Lucas Mwampiki, alijiuzulu nafasi zake kwa madai ya kwamba amechoka kuwa mtumwa wa fikra.

Uongozi wa chama yaani Mwenyekiti John Mwambigija na baadhi ya wenzake waliitisha vyombo vya habari n a kusema chama kilikuwa tayari kimemfukuza uongozi kabla ya kutangaza kujiuzulu kwake.

Usanii wa namna hiyo uliwahi kutokea kwa baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho akiwemo Katibu Mkuu wa kuchaguliwa, Eddo Mwamalala, ambaye kwa sasa ni kamishna wa NCCR-Mageuzi mkoa wa Mbeya.

Alisema  alipisha uongozi wa ubabaishaji na kuchoshwa na kuchonganishwa na wananchi na kwamba kama anataka kuwania Ubunge 2015 lazima aandike barua makao makuu. Chadema baada ya kuona hivyo, walitangaza kuwa alifukuzwa!

Kosa la Mwamalala lilionekana ni kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kumtaka katibu mkuu wa chama hicho taifa Dr. Wilbroad Slaaa, kujiuzulu baada ya kukiri kumiliki kadi ya CCM.

‘’Leo tarehe 03/01/2012 ni siku muhimu yenye kumbukumbu nyingi juu ya  maisha  yangu kisiasa. Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 kipengele cha 5.4 kukoma kwa Uanachama,  kifungu kidogo cha 5.4.1; nanukuu “ kwa kujiuzulu mwenyewe  kwa hiari yake.” Mimi Edo Makata Mwamalala leo hii naamua kutekeleza katiba hiyo; najiuzulu uanachama’’ alisema Mwamalala.

Kampeni meneja wa Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu), Anyandwile Mwalwiba, pia alitimuliwa kwa kosa la kumzuia Mbowe, kufungua tawi eneo la Sido Mwanjelwa Mbeya.

Kampeni meneja huyo ndiye aliyeanzisha propaganda ya kwamba aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Benson Mpesya (CCM),(DC KAHAMA kwa sasa), alikuwa akijenga vilabu badala ya shule. Alikuwemo pia Daniel Mwambipile na Solwa Ngela.

Barua za kuwafukuza uanachama viongozi hao, zilisainiwa na katibu wa Chadema Mbeya Mjini Christopher Mwamusiku.

Moja ya barua hiyo ni yenye kumbukumbu namba CDM/MBM/KUW/2012/12/40 ilimweleza Daniel Mwambipile kuwa kosa lake ni kushirikiana na Solwa na wengine na kufanikisha kumzuia Mbowe kufungua tawi la Sido Mwanjelwa.

''Kamati ya utendaji iliona makosa yako ni makubwaa na ya hatari kwa ustawi wa chama, hivyo iliamua kutoa adhabu ya kukufukuza uanachama na ilikutia hatiani kwa mujibu wa katiba ya Chadema ya mwaka 2006 sura ya kumi (x),(vii),(viii),(ix) na (xi)'' inasomeka barua hiyo.

Kwa upande wa Mshauri wa Chadema mkoa wa Mbeya ambaye pia alinyang'anywa wadhifa wake wa ukatibu wa chadema mkoa wa Mbeya na Dr. Wilbroad Slaa, mwanasheria Eddo Mwamalala, barua ya kufukuzwa uanachama baada ya kujiuzulu ni kutoa mara kwa mara matamko mazito kupitia vyombo vya habari.

Taarifa za kufukuzwa uanachama wanachama hao, zilithibitishwa na Katibu wa Chadema wilaya ya Mbeya mjini Christopher Mwamusiku.

Solwa Ngela mbali na sababu ya kumkataa Mbowe kufungua tawi la Sido, pia ilielezwa kuwa alikuwa akihamasisha ukabili kwamba viongozi waliopo kwa sasa wote ni kabila la Wanyakyusa na siyo wasafwa hivyo inatakiwa kuwe na usawa.

Alipohojiwa kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aliwahi kuhamasisha ukanda na ukabila hakufukuzwa lakini wao wameamua kuwafukuza wenzao, Mwamusiku alisema kosa la Nassari  na hawa wa Mbeya hususani Solwa yanatofautiana.

Baadhi ya wanachama na viongozi hao walirejeshwa na baraza la masuluhishi baada ya kubaini kuwa viongozi waliopo waliohusika na wanaendelea kuhusika kuwafukuza wenzao bila uhalali.

Hii ni taswira ya machache ambayo yanatokea ndani ya Chadema wilaya ya Mbeya Mjini na inaweza kuwa ndiyo taswira ya Chadema nchi nzima.

Nasema nchi nzima kwasababu, sababu za viongozi wengi wa chama hicho wanapoondoka au kujiuzulu zinafanana.

Wengi wanalalamika kuwa wamekijenga chama kwa gharama zao lakini hawathaminiwi hasa upande wa ruzuku na ajira za makao makuu. Chadema hawajawahi kupinga hoja za wanaotoka na wanaojiuzulu.

Serikali inatoa ruzuku kwa ajili ya kuendeleza demokrasia, lakini tatizo la suala la ruzuku kutokufika chini kwenye chama siyo la Chadema pekee bali hata kwa CCM, mabalozi wanalalamika pia.

Inashangaza kuona makatibu wa vyama vya siasa wanalipwa, wabunge wanalipwa lakini wanaojenga chama hawalipwi!

Kwa upande wa Chadema, sioni kama ni vema kuendelea kuwapuuza wanaoondoka ambao kila mmoja analaumu mtiririko wa watalawa wao.

Chacha Wangwe alilaumu uongozi, Dr. Kaburu wa Buzebazeba Kigoma Ujiji, Zitto Zuberi Kabwe wa Mwandiga njia panda barabara kwenda Manyovu Kigoma, Thomas Nyimbo wa Njombe, Juliana Shonza  na Mwampamba na msululu wa viongozi na wanachama wanalalamikia uongozi.

Ujasiri unaooneshwa na Chadema kuisimamia serikali, unashindikana ndani ya chama.

Je wanademokrasia wa kweli na wazalendo ni wale tu ambao wapo karibu na Mwenyekiti na Katibu wa Taifa?.

Natoa hoja

No comments: