Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, May 04, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 03.05.2014.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.


 


       R.P.C                                                                                          Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                           Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572                                                                                               S. L. P. 260,
Fax -+255252503734                                                                                               MBEYA.
E-mail:rpc.mbeya@tpf.com.tz
Unapojibu tafadhali taja 

                                                                     

YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 03.05.2014.

·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

·         MWANAMKE MMOJA AUAWA KWA KUCHOMA KISU SEHEMU MBALIMBALI NA MUME WAKE.

·         WATU WAWILI WAFA MAJI BAADA YA MTUMBWI WALIOKUWA WAKIUTUMIA KUZAMA.


·         RAIA NA WAKAZI 02 WA NCHINI ETHIOPIA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIB ALI.


·         WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUPATIKANA NA BHANGI KATIKA MATUKIO MAMWILI TOFAUTI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AITWAYE ANAHERI LAZARO (43) MKAZI WA MPOLO AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KATIKA BEGA LA KULIA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUTUMIA BUNDUKI AINA YA GOBOLE WAKATI WAKIWA KILABUNI WAKINYWA POMBE ZA KIENYEJI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPOLI- IGAWA, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI. KATIKA ENEO LA TUKIO KUMEOKOTWA GOLOLI MOJA YA GOBOLE. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO HAKIJAFAHAMIKA. MWILI WA MARFEHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI. WATU SITA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO/WALIPO MTUHUMIWA/WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA REHEMA IVOD SICHELA (22) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE AITWAYE GASPER ATHANAS MKAZI WA IVUNA WAKIWA NYUMBANI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA IVUNA, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

 INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMTUHUMUMAREHEMU MKE WAKE KUWA SIO MWAMINIFU KATIKA NDOA YAO. MTUHUMIWA AMBAYE ANA WAKE WAWILI ALIKIMBIA NA MKE MKUBWA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.


KATIKA TUKIO LA TATU:
WATU WAWILI WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA DIPLPOMA YA BUSSINESS ADMINISTRATION CHUO CHA MZUMBE KAMPASI YA MBEYA, WAKAZI WA FOREST YA ZAMANI HOSTELI ZA NJE WALIOTAMBULIWA KWA MAJINA YA 1. MICHAEL TARIMO (20) NA 2. ALBERT SHENKALWA (23) WALIKUFA MAJI BAADA YA MTUMBWI WALIOKUWA WANAUTUMIA KUPIGWA MAJI, KUPINDUKA NA WAO KUSHINDWA KUOGELEA. 

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA ZOO YA WANYAMA ILIYOPO KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – KATA YA SONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJIJINI. WANAFUNZI HAO WAKIWA NA WENZAO 12  WALIKWENDA ENEO HILO KWA AJILI YA  PICKNIC NA KUANGALIA WANYAMA NA BAADAE KWENDA KWENYE BWAWA LINALOTUNZA SAMAKI NA KUANZA  KUINGIA NDANI  YA  BWAWA HILO KWA KUTUMIA MTUMBWI HUO KWA ZAMU. 

KATIKA BWAWA HILO WATU HAWARUHUSIWA KUOGELEA ISIPOKUWA KUINGIA KWA MTUMBWI.  


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MAZINGIRA WANAYOKWENDA KUTEMBMELEA ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

KATIKA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WAWILI WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.


KATIKA MSAKO HUO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA TUKUYU MJINI, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA  RUNGWE,  MKOA WA MBEYA WAHAMIAJI HARAMU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LILE ROSE (20) NA 2.  SAMWEL TAKTAN (20) WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WALIKAMATWA NA KISHA KUKABIDHIWA IDARA YA UHAMIAJI KWA TARATIBU ZAIDI ZA KISHERIA.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI WAONAPO WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE.


KATIKA MSAKO WA PILI:
WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI. KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA MIGOMBANI-TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA,   WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA YA SAA 12:40 MCHANA WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. HASSAN KUFAKUNOGA (25) MKAZI WA KALOLENI 2. MLOTWA SIMTENDA (30) MKAZI WA NAKONDE -ZAMBIA NA   3.  ELISHA MWAMBENE (24) MKAZI WA NAKONDE-ZAMBIA WAKIWA NA BHANGI KETE 241 SAWA NA UZITO WA KILO 1 NA GRAMU 205.

AIDHA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA MIGOMBANI-TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA,   WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 02.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. PETTER SIAME (19) MKAZI WA KALOLENI NA 2. FRANK MWAMBENE (24) MKAZI WA KALOLENI WAKIWA NA BHANGI GRAM 500 NA KETE 19 SAWA NA UZITO WA GRAMU 595. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA WOTE ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: