Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, May 04, 2014

WASOMI MZUMBE WAFA MAJI WAKIOGELEA

IMG_0269

WANAFUNZI wawili waliokuwa wakisoma katika Chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya, wamekufa maji wakati wanaogelea na mitumbwi katika bwawa la samaki lililopo katika hifadhi (zoo)ya wanyama Ifisi inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, Mbeya Vijijini.

Kamanda wa polisi Ahmed Msangi, aliwataja marehemu kuwa ni Michael Tarimo(20), Albert Shenkalwa(23) na kwamba wanafunzi hao walikuwa mwaka wa kwanza katika chuo hicho wakisomea uongozi wa biashara ngazi ya Stashahada.

“Walikuwa 12, walikwenda picknic kwa ajili ya kuangalia wanyama, baadaye kwenda kwenye bwawa linalotunza samaki na kuingia kwenye maji kwa zamu na mitumbwi, Mtumbwi waliokuwa wakiutumia ukapinduka na wao kushindwa kuogelea’’ alisema Kamanda Msangi.

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo la chuo hicho na kuwakuta wanafunzi wakiwa na huzuni huku wakiwa wamavaa mavazi ya staha kuliko siku zingine zote.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Jackob Mwakasole, alisema tukio hilo lilitokea Mei 2, mwaka huu katika eneo hilo na kuleta simanzi kubwa.

Alisema madimbwi hayo ni maalum kwa ajili ya kuhifadhi samaki na maji ya mvua kwa ajili ya wanyama wanaotunzwa katika eneo hilo, lakini ajabu wanafunzi hao waliingia na kuanza kuogelea.

“Tumepata simanzi kubwa, kwasababu bwawa walilojitosa kuogelea ni kwa ajili ya kufugia samaki na maji ya wanyama. Ni maji ambayo kwa akili ya kawaida mtu mzima hawezi kuingia kuogelea, tulifanya jitihada za kuopoa miili kwa kuanza kupunguza maji kwa mashine tukishirikiana na Mkurugenzi wetu Mch.Marcus Lehner, vijana wanaojua kuogelea na kuzamia, askari polisi na wasamaria wema wengine ’’ alisema Mwakasole.

Alipoulizwa kuwa ilikuwaje marehemu waliruhusiwa kuingia katika bwawa hilo, alisema katika eneo hilo kuna mitumbwi midogo kwa ajili ya kuvulia samaki na kupiga picha, lakini walimshawishi mtumishi mmoja wa hifadhi hiyo kuwa wao walikuwa na utaalam, jambo ambalo kumbe halikuwa sahihi.

“Walikuwa na mabinti kadhaa, tulikuta eneo la tukio mabaki ya vinywaji kama Juice na karatasi za pombe kali na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nao pia tuliwakuta eneo hilo’’ alisema Mwakasole.

No comments: