Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, October 06, 2014

BINTI ATESEKA DAR ES SALAAM, ATAMANI KUMWONA MAMA YAKE ALIYEKO MBEYA

KHADIJA (MOSA) Juma Mrisho, anayeishi mitaani Jijini Dar es Salaam, anaomba msaada wa kumpata mama yake mzazi aliyepo mkoani Mbeya.

 
Anahitaji msaada huo kutokana na mateso anayoyapata mitaani, ikiwa ni pamoja na kutendewa vitendo visivyo vya utu.

Kila atakayeguswa kwa nia ya kumsaidia, hasa wenye vyombo vya habari vinavyosoma na kusikika(redio), mkoani Mbeya, hapa chini ni waraka wa binti huyo, ambao unaweza kusomwa au kuandikwa kwa nia ya kumuunganisha na mama yake.

 NAMTAFUTA MAMA YANGU ANAYEITWA JANE 
Jina langu naitwa Hadija na jina langu la utoto naitwa Mosa. Jina la baba yangu anaitwa Juma Mrisho kabila lake Mnyamwezi. 

 
Mama yangu anaitwa Jane jina la baba yake silikumbuki. Kabila la mama yangu ni muwanji,msafa.  

Nilizaliwa Mwanjelwa, mkoani Mbeya mwaka 1985. 

Nilipofikisha umri wa miaka mitano(5) baba na mama walitengana, nikachuliwa na baba yangu kwa njia ya kunitorosha kutoka Mbeya akanipeleka  Sikonge,Tabora kwa bibi ambaye ni mama yake baba. 

Bibi yangu anaitwa Hadija Iddi Mhozya. 

Baba aliniacha kwa bibi yangu  na yeye akaondoka pasipo mimi kujua alikwenda wapi sababu nilikuwa mdogo. Bibi yangu aliniambia baba yangu aliondoka kwenda kutafuta maisha. 

Sikuonana na baba yangu kwa muda wa miaka mingi na badaye  nilikuja kuonana na baba mwaka 2008 Kibaha Dar es salaam, mimi wakati huo nikiwa na umri wa miaka 23.  

Lakini wakati huo wote nilikuwa nikimwuliza bibi yangu mama yangu yuko wapi, bibi alikuwa akinieleza mama yangu yuko mbeya anaitwa Jane. 

Mwaka 2005 niliamua kwenda kumtafuta mama yangu mbeya nikampata akiwa anaishi maeneo yanaitwa ILEMI DARAJANI, Mwanjelwa , Mbeya .  

Nilikaa na mama yangu muda wa wiki moja nikaondoka.  Baadaye mimi na bibi tulihamia kwa baba kibaha nikaendelea kuishi na bibi baadaye bibi alifariki na baadaye baba alifariki pia na mimi sikuwa na sehemu tena  ya kuishi na sikupata nafasi ya kusoma shule, ndipo nikaanza maisha ya taabu ya kujitafutia riziki mwenyewe.  


Nimepitia mambo mengi ya taabu na shida, kubezwa na kudharauliwa na jamii kwasababu ya maisha yangu ninayoishi  ya mitaani.  

Sijawahi kupata msaada wowote kwa ndugu wa baba yangu wala mama yangu kunitafuta.

Kwasababu ya maisha  magumu  kuendelea  ya kujitafutia riziki mitaani mwenyewe sijaweza  kupata fedha ya kutosha nauli kwenda mbeya kumtafuta mama yangu kwa vile  napata riziki ya kula tu.

Pia sina hakika kama mama yangu bado yupo mbeya au alishahama au sijui kama yupo hai.  

Nimeamua kumtafuta mama yangu kama yupo hai ili tuweze kuishi pamoja, naumia kutomwona mama yangu na kutojua kama bado anaishi au hapana. 

Nimeamua kupitia redio hii  kumtafuta.  Kama kuna mtu yeyote ambaye anajua mama yangu alipo au kama mama atapata nafasi ya kusikia kwenye redio apige namba ifutatayo: 0764168544. 

MAMA NAKUTAFUTA NATESEKA hata kama uliolewa na mwanamume mwingine mimi ni mwanao nahitaji tuwasiliane ni kuone mama.

Mimi Hadija (Moza) Juma Mrisho – MWANAO MAMA NAKUTAFUTA NINA HUZUNI MNO KUKOSA BABA, MAMA.

Pia naishukuru  hii kwa kunisaidia kurusha taarifa hii ili nimpate mama.

No comments: