Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, October 25, 2014

CHIDI BENZI AKAMATWA NA POLISI, ATUHUMIWA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE

Chid Benz
DSM Airport
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram Party inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.
Msanii huyu amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo; baada ya kukamatwa alifanyiwa upekuzi na kubainika akiwa na misokoto miwili ya bangi na kete 14 za dawa hizo dawa za kulevya zilizokutwa kwenye mfuko wa shati lake.
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani ambae ni kamanda wa polisi wa viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha kukamatwa kwa Chidi Benz aliyehojiwa na kukiri dawa hizo ni zake.
Selemani amesema “alikuja Airport kwa ajili ya safari kwenda Mbeya; alikutwa na, kete hizo 14 za dawa za kulevya zikiwa zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye mwenyewe amekiri ni vitu vyake anavyovitumia.”
Katika mahojiano na Polisi, Chid Benz anaelezwa kushangaa kwanini dawa hizo zilikuwa kwenye mfuko wa shati lake.

Selemani amesema Chidi Benz atafikishwa mahakamani wakato wowote kuanzia sasa mara tu baada ya kubaini aina ya dawa hizo za kulevya.
chanzo;millardayo.com 


No comments: