Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, October 21, 2014

DIWANI CCM AZUIA MAITI YA MWANAE ISIZIKWE, MGOGORO WAINGIA SIKU YA 47Na Charles Ndagulla,Moshi

WINGU  zito limetanda juu ya hatima ya mazishi ya Rosemary  Marandu(38) aliyefariki dunia septemba 4 mwaka huu kutokana na kuwapo kwa sintofahamu ya nani hasa mwenye haki ya kuuzika mwili huo.

Mwili huo ambao jana umerfikisha siku  46 ukiwa unaendelea kuhifadhiwa katika hospital ya rufaa ya KCMC,umekwama kuzikwa kutokana na kuwapo na mgororo wa kifamilia ukimhusisha baba mzazi wa marahemu,Flavian Marandu na familia yake akiwamo mkwewe,Sigfrid Mlingi.

Mume huyo wa marehemu anamtuhumu baba mkwe wake kwamba ndiye aliyezuia mwili wa mkewe mpendwa usizikwe huku Marandu mwenyewe akikana tuhuma hizo.

Akizungumza na mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com mwishoni mwa wiki, Marandu ambaye ni diwani wa kata ya Mrao Keryo(CCM) wilayani Rombo, alikana tuhuma hizo akidai kuwa hawezi kuingilia mazishi na mke wa mtu.

Marandu ambaye ni mfabiashara anayemiliki vitega uchumi kadhaa katika miji mbali mbali hapa nchini, vikiwamo viwanda vya kupasua  mbao, amedai kuwa anachofahamu yeye ni kwamba mwanye marehemu Rosemary anaye mume wake hivyo isingekuwa busara yeye kuingilia taratibu za mazishi.
 
Marandu amesisitiza kuwa,ametoa Baraka zote kwa ndugu  na jamaa pamoja na mume wa maremhemu mwanaye wa kuchukua kibali cha mazishi na kwenda kuzika wanakoona panafaa lakini wanandugu wangali na hofu juu ya kauli hiyo.
 
Wakati  mfanyabiashara  huyo akikana madai hayo,mume wa marehemu amesisitiza kuwa mwili wa mkewe umezuiliwa na baba mzazi wa marehemu huku  akidai kuwa, yote anamwachia mungu.

Mlingi amedai kuwa,baada ya kifo cha mkewe alikwenda  nyumbani kwa baba mkwe wake katika kijiji cha Mrao Keryo ili kuweka sawa mipango ya mazishi lakini anadai kufukuzwa na kutolewa lugha isiyokuwa na staha.

Alisema alimuuguza mkewe katika Hospital ya mkoa ya mawenzi hadi alipomfia mikononi mwake lakini akasikitishwa na kauli za kuuzi alizozipata kutoka kwa baba mkwe wake

Mwili huo  wa  marehemu Rosemary Marandu  umekuwa ukilipiwa sh,9,000 kila siku kama gharama za kuuhifadhi na jana olipofika siku ya 46 ulihitajika kulipiwa kiasi cha Tsh.414,000/=
 
Kwa mujibu wa mume huyo wa marehemu,awali kulikuwapo na makubaliano ya kuuzika mwili wa maremhemu mkewe katika makaburi ya umma eneo la karanga mjini hapa septemba 9 lakini  baba wa marehemu alibadili msimamo na kukataa.


 Mgogoro huu unaibuka siku chache baada ya mgogoro mwingine wa kugombea mwili wa marehemu Steven Laurent Assey, aliyefariki dunia  septemba mosi katika Hospital ya taifa Muhimbili, kuhitimishwa septemba 30 na mahakama ya hakimu mkazi mjini moshi .

Mgogoro huo ulihusisha wake wawili wa marehemu Assey,Lucy Assey na Fortunata Lyimo ambako mke wa kwanza wa marehemu,Lucy Assey alikuwa akipinga mke mwenzake kuzika mwili huo akidai hana haki hiyo.

Lakini mahakama  chini ya hakimu Munga Sabuni, ilihitimisha mgogoro huo septemba 30 baada ya kumpa haki mke mdogo wa maherehmu  ya kuzika mwili huo baada ya ushahidi kubaini kuwa marehemu aliacha wosia wa mdogo kuwa akifariki azikwe Kilema chini eneo la Masaera nyumbani kwa mke mdogo.
 
 
Akitoa umauzi huo ,hakimu  Sabuni,alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya wosia wa mdomo ya mwaka 1963 kama ilivyotangazwa kwenye gazeti la serikali namba 436,marehemu Assey alitimiza matakwa ya sheria hiyo kwa kuita watu wanne na kuwapa wosia wa mdomo kuhusu eneo analotaka azikwe endapo atafariki.

No comments: