Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, October 04, 2014

KAMANDA WA POLISI MBEYA, AHMED MSANGI, AWA MGENI RASMI MECHI YA PRISON NA AZAM SOKOINE MBEYA MUDA HUU.

 Baadhi ya wachezaji wa timu ya AZAM FC kutoka jijini Dar es Salaam, wakiwa uwanja wa sokoine Mbeya leo.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, akikagua timu ya azam Fc na Tanzania Prison, jioni ya leo uwanja wa sokoine Mbeya.
 Baadhi ya watangazaji wa radio ya Mbeya Highland ya Jijini Mbeya, wakiwa wanarusha matangazo ya mechi kati ya Tanzania Prison na Azam FC.
 Baadhi ya mashabiki wakiwa uwanjani sokoine Mbeya, wakishuhudia mchezo wa Tanzania Prison na Azam FC.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, akiwatakia kheri wachezaji wa Tanzania Prison na Azam Fc, huku akiwasisitiza kuwa ni vema kuwa na fear pray.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA), Elias Mwanjala, wakitoa uwanjani kugagua timu za Tanzania Prison na Azam Fc, hapa uwanja wa sokoine Mbeya, jioni ya leo.
 Baadhi ya watoto kati ya miaka mitatu mpaka mitano, wa kituo cha Mbeya Umoja Sports Academy ya Uyole Jijini Mbeya, chini ya Mkurugenzi wa kituo hicho Deus Nsheka, wakiwa katika jukwaa la Tanzania Prison, wakishuhudia mechi kati ya Tanzania Prison na Azam Fc, Katika uwanja wa sokoine Mbeya, jioni ya leo. Ambapo mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa bado hazijafungana.
 Kulia ni mpenzi wa michezo mkoani Mbeya, Ayas Yusuph, akiwa pamoja na Mkurugenzi wa kituo cha Mbeya Umoja sports Academy, Deus Nsheka, katika jukwaa la Tanzania Prison, wakati wa mechi ya timu hiyo na Azam Fc, jioni ya leo hapa uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA), Elias Mwanjala, waiingia kukagua timu ya Tanzania Prison na Azam fc, wakati wa mechi ya timu hizo hapa uwanja wa sokoine Mbeya, jioni ya leo.

No comments: