Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, October 29, 2014

MBEYA CITY WASAKWA KWA KOSA LA SHAMBULIO SIKU chache baada ya mashabiki wa timu ya Mbeya City ya Jijini Mbeya, kutuhumiwa kufanya fujo katika uga wa sokoine kutokana na timu yao kufungwa goli mbili na timu ya Mtibwa suger, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo nao wameingia matatani kwa tuhuma za kumshambilia dereva Jonathan Solomon(31), wa kampuni ya pepsi Jijini hapa.Tukio hilo limetokea jana Octoba 28, mwaka huu, eneo la Sokomatola, baada ya wachezaji wa timu hiyo kushuka kwenye gari walilokuwa wakisafiria na kuanza kumshambulia kijananhuyo.Inadaiwa kuwa, baadhi ya wachezaji hao, walishuka na kuanza kumhoji dereva huyo kwamba kwanini aliegesha gari lake vibaya, na alipoomba kuegesha vizuri akaanza kupigwa.Gazeti hili lilizungumza na mhanga wa tukio hilo, ambaye alifika katika kituo kikuu cha polisi na kutoa taarifa kisha akapewa fomu namba tatu(PF3), na kwenda kutibiwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya.Alipohojiwa, Jonathan, alisema kuwa alikuwa akiteremsha soda eneo la Kalembu Bar, ndipo likaja gari la wachezaji hao ambao walimwamuru aegeshe vema gari lake na alipoingia na kuwaomba wasogeze nyuma gari lao ndipo akaanza kupigwa.“Niliwatambua wachezaji wawili kati ya walionipiga, alikuwepo Steve na Deus na kunijeruhi mdomo wangu huku wakipasua chupa za soda na baada ya shambulio fedha taslimu 631,800/=, zilikuwa kwenye gari nililokuwa nikiendesha lenye namba T 544 ATP aina ya Mazda, sijazikuta na ndipo nikaenda polisi” alisema Jonathan.Taarifa iliyopokelewa polisi ni shambulio, ambalo limefunguliwa jarada namba MB/IR/8648/2014.

No comments: