Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, October 14, 2014

MUWSA KWAFUKA MOSHI, MAGHEMBE AAGIZA UCHUNGUZI


 
 
Na Charles Ndagulla,Moshi .

HALI  si swari ndani ya Mamlaka ya maji safi na uondoshaji maji taja(MUWSA) baada ya wafanyakazi kuibua madudu mengi yanayofanywa na uongozi wa mamlaka hiyo.

Miongoni mwa madudu hayo ni ubaguzi katika suala la malipo ya wafanyakazi ambako taarifa zinadai kuwa, kipaumbele kimekuwa kikitolewa kwa wafanyakazi waliotoka DAWASCO ambako mkurugenzi wa sasa wa mamlaka hiyo,Cyprian Luhemeja alitoka huko.

Katika andiko lao,wafanyakazi hao wanadai kuwa,hata taarifa za upotevu wa maji ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na mamlaka hiyo si sahihi huku mishahara ikidaiwa kutolewa bila kuzingatia viwango vya elimu.

Aidha wafanyakazi hao wamedai katika andiko lao kuwa,wapo wateja wapya wapatoa 200 hawajaunganishiwa huduma ya maji kutokana na wazabuni kutolipwa malipo yao kwa wakati.

Wafanyakazi hao wameonya kuwa,kutokana na kuyumba kwa mamlaka hiyo,ipo hatari kwa mamlaka hiyo kushuka hadhi yake na kurudi daraja B kutoka daraja A kutokana na mishahara ya watumishi kusuasua.

Madai mengine ya wafanyakazi hao ni matumizi mabaya ya fedha za mamlaka ambako,yamekuwa yakifanyika manunuzi ambayo hayafuati taratibu na sheria ya manunuzi wakitolea mfano wa manunuzi ya mapazia yaliyofanywa na mtu mmoja(jina tunalo)wakidaI tararibu zilikiukwa.

Kutokana na tuhuma hizo,waziri  wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe,ameiagiza bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na uondoshaji majitaka moshi  mjini(MUWSA) kuchunguza malalamiko ya wafanyakazi hao.

Maghembe ametoa maagizo hayo hivi karibuni alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuwepo kwa taarifa za kuwapo na mgongano wa kimaslahi na ubaguzi wa kada ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa MUWSA,Shally Raymond,alikiri kuwapo kwa malalamiko hayo ya wafanyakazi na kwamba tayari uchunguzi umeanza kufanyika.

Mwenyekiti huyo ambaye amewahi kuwa mbunge wa viti maalum(CCM) na meneja wa CRDB tawi la moshi,alijibu kwa ufupi kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya kiganjani alipoulizwa.

“marahaba,asante,kama ulivyoelezwa,jambo hili linafanyiwa kazi,asante sana kwa ushirikiano,usiku mwema”ulisomeka ujumbe mfupi wa maandishi uliotumwa na mwenyekiti huyo kwa mwandishi wa bahari hizi.

No comments: