Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, October 27, 2014

MWENYEKITI UVCCM CHUNYA, SAUL MWAISENYE, AWAZAWADIA WANAFUNZI


 Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Chunya Saul Mwaisenye akizungumza wakati wa ufunguzi wa baraza la vijana Wilayani humo hivi karibuni.


MWENYEKITI wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM), wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Saul Mwaisenye, amewazawadia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wapatao 100, katika baadhi ya kata wilayani humo.

Katika ziara yake ya kikazi kijijini Mlimanjiwa, wilayani hapo, aliyoifanya juzi, Mwaisenye, aliwazawadia watoto hao madaftari manne kila mmoja, penseli, biki, pamoja kula nao chakula.

Akipokelewa na vikundi saba vya akina mama wajasiliamali, ambao wanatumia ujasiliamali wao kusaidia watoto na wazazi wasiojiweza, alichangia kiasi cha fedha Tsh.350,000/= na daftari 200.

“Kutoa siyo utajiri, bali kama mkazi na kiongozi, lazima nijumuike katika shughuli hizi za kijamii na kurejesha fadhila zangu kwa jamii niliyokulia” alisema Mwaisenye.        

No comments: