Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, November 06, 2014

AKAMATWA KWA KUWAUZIA WENZAKE NYAMA YA MBWA
MTU mmoja amekamatwa na Jeshi la polisi baada ya kuwauzia wananchi wenzake kitoweo cha Nyama ya Mbwa.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa vyombo vya habari LEO, imesema kuwa, jeshi hilo linamshikilia kijana Ahadi Jesikaka(20), ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ngyekye wilayani Kyela kwa kosa la kuwauzia watu nyama ya mnyama huyo.

 Taarifa hiyo iliyosainiwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi, imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea Novemba 4, mwaka huu. ‘’Tukio hilo limetokea tarehe 4.11.2014, majira ya saa saba mchana, huko katika kijiji cha Ngyekye, kata ya Matema, tarafa ya Ntebela wilaya ya Kyela mkoani Mbeya” imeeleza taarifa hiyo.

Watu waliouziwa na kutumia kitoweo hicho cha nyama ya Mbwa ni Enock Nsemwa(52), George Nsemwa(26) na Anyandwile Mbwilo(29), wote wakazi wa Ngyekye. Kutokana na tukio hilo, jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa makini hususani wanaponunua vyakula ili kujiepusha na madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza.

Chanzo;Make money by copying the best: http://bit.ly/copy_win
AKAMATWA KWA KUWAUZIA WENZAKE NYAMA YA MBWA MTU mmoja amekamatwa na Jeshi la polisi baada ya kuwauzia wananchi wenzake kitoweo cha Nyama ya Mbwa. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa vyombo vya habari LEO, imesema kuwa, jeshi hilo linamshikilia kijana Ahadi Jesikaka(20), ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ngyekye wilayani Kyela kwa kosa la kuwauzia watu nyama ya mnyama huyo. Taarifa hiyo iliyosainiwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi, imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea Novemba 4, mwaka huu. ‘’Tukio hilo limetokea tarehe 4.11.2014, majira ya saa saba mchana, huko katika kijiji cha Ngyekye, kata ya Matema, tarafa ya Ntebela wilaya ya Kyela mkoani Mbeya” imeeleza taarifa hiyo. Watu waliouziwa na kutumia kitoweo hicho cha nyama ya Mbwa ni Enock Nsemwa(52), George Nsemwa(26) na Anyandwile Mbwilo(29), wote wakazi wa Ngyekye. Kutokana na tukio hilo, jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa makini hususani wanaponunua vyakula ili kujiepusha na madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza.

Make money by copying the best: http://bit.ly/copy_win

No comments: