Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP, Liberatus Sabas(kulia)
 
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Olkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amefanyiwa ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na kuondolewa kiganja cha Mkono, sikio na sehemu nyingine za mwili wake.
 
Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Paulina Joseph amefanyiwa ukatili huo na mtu anayedaiwa kuwa ni shemeji yake kwa madai ya kuingilia ndoa yake.
 
Tukio hilo lilimkuta bi Paulina akiwa shambani kwake akikata nyasi kwa ajili ya kulisha mifugo.
 
Mume wa Paulina ameeleza masikitiko yake kwa uongozi wa kijiji,Kitongoji na kata kwa kushindwa kumkamata mtuhumiwa na kutoroka kwani kitendo hicho kinaweza kusababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatii dhidi ta wanawake nchini.
 
Viongozi wa kijiji hicho wamekanusha kuwa hakuna uzembe uliofanyika kumkamata mtuhumiwa huyo kwani bado inaendelea kumtafuta na kumtia hatiani.
 
Bi Paulina anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital Teule ya Seriani wilayani Arumeru alipolazwa na hali yake bado sio nzuri.