Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, November 07, 2014

NDEGE YA RAIS WA CHINA YAHUSISHWA NA WIZI WA PEMBE YA NDOVU


Rais wa nchi ya China, Xi Jinping akiwapa mkono wananchi wa Tanzania.
Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya binafsi ya Rais wa Uchina, Xi Jinping wakati alipozuru bara Afrika. Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London.
Ndege ya rais wa China.
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa China kuja nchini tanzania mwaka ulioipita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa.
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Pembe za ndovu.
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu. (CREDIT: BBC SWAHILI)

No comments: