Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, November 06, 2014

SAUTI KUTOKA NYIKANI...... AMANI KAJUNA, MWENYEKITI WA UVCCM MBEYA ANAYETAJWA KUMRITHI SUGUMake money by copying the best: http://bit.ly/copy_winMake money by copying the best: http://bit.ly/copy_win

NA GORDON KALULUNGA

WIKI iliyopita tuliona wasifu wa mwanafunzi wa chuo cha kodi Jijini Dar es Salaam, Nwaka Mwakisu, ambaye ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM na UVCCM Taifa akitokea mkoa wa Mbeya, ambaye pia anatajwa kutaka kupeperusha bendera ya CCM ngazi ya Ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini lililopo chini ya Joseph Mbilinyi(Sugu) wa Chadema.

Awali tulitazama wasifu wa kijana Eliurd Mwaiteleke, ambaye ni kamanda wa UVCCM kata ya Sinde Jijini Mbeya na leo kurunzi la sauti ya Nyikani, linamwangaza Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM(UVCCM), Mkoa wa Mbeya, Mwalimu Amani Kajuna, ambaye pia ni mmiliki wa shule ya mchepuo wa kiingereza, The Shinning School, iliyopo wilaya ya Mbeya.

Kiongozi huyu wa vijana wa CCM mkoa wa Mbeya, mara kadhaa ananukuliwa akisema kuwa kuanzisha shule ni zao la mawazo yake ya kutaka kurudisha fadhila kwa watanzania kutokana na historia ya maisha yake ambayo amelelewa akiwa yatima na kusomeshwa, hivyo anaamini kwamba bila elimu hasa elimu ya vitendo hakuna mtanzania atakayeweza kuimarika kiuchumi.

‘’Kujikita katika elimu ni fadhira ninazotaka kurudisha kwa watanzania wenzangu kwasababu najua wazi kuwa bila elimu hasa elimu ya vitendo na kama serikali haitakuwa macho na mfumo wa elimu uchumi wa nchi utashuka’’ ananukuliwa Kajuna hata katika mahojiano ya mwaka 2011 na mwandishi wa makala haya.

Anasema alipohitimu darasa la saba alifanikiwa kujiunga na shule ya Musoma Tech School, ambayo ilikuwa inatoa elimu ya ufundi kwa wanafunzi, tofauti na sasa shule za namna hiyo zinatoa zaidi elimu ya nadharia, jambo ambalo linasababisha Taifa kupoteza wataalam na kusababisha kushuka kwa uchumi utokananao na wataalam wa ndani.

Kajuna, ambaye pia ana taaluma za siasa na Diplomasia anaweka wazi historia ya maisha yake kuwa Baba yake mzazi alifariki yeye akiwa na umri wa miaka  mitatu na baadaye akiwa na umri wa miaka sita, Mama yake pia alifariki dunia, hivyo akabaki mikononi mwa Bibi yake, Angelina Aman, mkoani Kagera, ambaye pia amefariki dunia mwaka huu.

Anatanabaisha kuwa, baada ya maswahibu hayo, alipata shida na kumpelekea kuanza kuponda kokoto, kukata nyasi na kuziuza na kucheza ngoma za asili kwenye misiba ili kupata mlo akiwa na Bibi yake mlezi.

Anasema licha ya kumshukuru Bibi yake aliyemlea, pia anamshukuru Mzee Pelesi Wandembe aliyemsaidia katika kupata elimu, shirika la PARTAGE la Ufaransa lililokuwa limejikita kusaidia watoto yatima mkoani Kagera,  kwa kutoa misaada ya kuwasomesha na hiyo anasema ni dira ambayo hataisahau katika maisha yake na walezi wake wengine ambao ni Alan Stokes na mkewe Vibienne Stokes ambao anasema kuwa wako naye bega kwa bega.

Mwaka 2012, Kajuna aliwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa(NEC) katika uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), wilaya ya Mbeya Vijijini, kura hazikutosha dhidi ya mpinzani wake, Fredy Towanga, huku baadhi wakisema kuwa ni kutokana na kwamba yeye si kabila la wilaya hiyo wala mkoa wa Mbeya.

Hoja ambayo ikawa dhaifu kwa baadhi ya vijana ambao mwaka huo huo, wakampa kura za ndiyo, katika nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya dhidi ya mpinzani wake mkuu, Mariam Mwaijumba.

Kijana huyu hajaanza siasa mwaka 2012, bali ameanza kabla ya hapo na mwaka 2010, aliwahi kuwania nafasi ya ubunge ndani ya CCM, huko mkoani Kagera.

Kuhusu kutajwa kwake kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbeya mjini, kunatokana na baadhi kuamini kuwa, katika jimbo hilo hakuna ukabila kama ulivyo Jimbo la Mbeya Vijijini, linaloongozwa na Mch. Luckson Mwanjale, ambako wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa yeye (kajuna) ameelekeza zaidi nguvu zake za nia ya kuwania nafasi hiyo.

Kutokana na uwezo wake wa kifedha, anatajwa kuwa itakuwa vema akawania nafasi hiyo kupitia jimbo la Mbeya mjini, kuliko kupoteza nguvu kubwa za nia yake katika Jimbo la Mbeya Vijijini, kwa madai kwamba yanaweza kumpata yale ambayo yaliwahi kumpata aliyekuwa Meneja wa kiwanda cha Saruji cha Songwe, Jovita Diame, licha ya matapeli wa siasa kumwaminisha kuwa alikuwa anakubalika.

Kinachotajwa kumponza Diame ni kuamini kuwa maendeleo aliyokuwa akiyafanya katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo na kuwa na fedha, basi ilitosha kuwashawishi wapiga kura ndani ya CCM kumpatia kura za ndiyo, jambo ambalo halikuzaa matunda kwa vipindi viwili alivyotumbukiza kete yake.

Huo ni mfano mdogo, ambao wanautumia kutoa tahadhali za nafasi ya Ubunge kwa kijana huyo na wengine wakiwemo wazawa wanaoishi Jijini Dar es Salaam na wasio wazawa.

Kwa sasa Kajuna, katika suala la siasa, anatamani zaidi kuendeleza suala la elimu na kwamba atahakikisha kufikia mwaka 2017 atakapomaliza uongozi wake wa UVCCM, anaibua na kuacha miradi ya kimaendeleo kwa kushirkiana na kamati yake ya utekelezaji ya mkoa wa Mbeya na wajumbe wote wa Baraza la vijana mkoani Mbeya.

Huyo ndiye Amani Kajuna. Tutawaletea kuwafahamu wengine kutokana na mahitaji ya watu wa nyikani, wiki ijayo tutatazama jinsi CCM inavyopanda na kutunguliwa katika mkoa wa Mbeya, mikoa mingine na ndani na nje ya chama chenyewe.

No comments: