Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, November 29, 2014

WAMA KUENDELEA KUWASOMESHA WATOTO WA KIKE BILA KUJALI AFYA ZAO


TAASISI ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA) inayoendeshwa na mke wa Rais, Mama Salama Kikwete itaendelea kuwasomesha watoto wa kike walio kwenye mazingira magumu bila kujali afya zao.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya kupambana na tatizo la kansa ya shingo ya kizazi, Mkurugenzi wa Maboresho ya Afya wa taasisi hiyo ya WAMA, Dk Sarah Maongezi alisema jukumu la taasisi hiyo ni kuhakikisha watoto wa kike wanapata haki ya elimu, ili kutimiza ndoto zao.

Maongezi alilazimika ufafanuzi kuhusu madai yanayotolewa na watu kwamba inasomesha maelefu ya wanafunzi, hasa wa kike, wanaodaiwa kuwa na maambukizi ya  virusi vya Ukimwi (VVU) kwamba hata hao wakiwepo wanahaki ya kupatiwa elimu, kama ilivyo kwa watu wengine.
“Taasisi hii itaendelea kuwasaidia watoto wa kike kwa kuwasomesha, hawa ni wale walio kwenye mazingira magumu wakiwemo yatima. Kumpima motto sio jukumu la WAMA, ila kazi yetu ni kuhakikisha anapata haki yake ya msingi ya kupatiwa elimu,”alisema Maongezi.
 
Alisisitiza kuwa kila mwaka wamekuwa wakipata watoto watatu kutoka kila mkoa kwa ajili ya kuwasomesha huku idadi kubwa ya watoto hao wa kike, ikitokea vijijini.
 Kutokana na kasi ya wanaume, wenye tama kuwazingira  wachuo wa kike wanaosoma kwenye vyuo vikuu vya mjini Iringa, kikiwemo Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) zamani kilijulikana kama Tumaini Iringa, Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa zilivuma habari za kuwepo kwa watoto wengi wakike wenye VVU ili kukomesha tabia hiyo.
 
“Kwa sababu watoto wa kike walikuwa hawasomi, kila siku magari ya kifahari yalizunguka vyuoni hasa nyakati za jioni, zikavuma taarifa za taasisi ya WAMA kumwaga watoto wa kike wenye VVU kwa lengo moja tu la kuwakomesha wanaume hao,” alisema.
 
Credit;mwitikio blog

No comments: