Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, December 06, 2014

FIESTA YAPONGEZWA

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya bia Serengeti, Steven Gannon, amepongeza tamasha la Fiesta linalofanyika kila mkoa nchini kila Mwaka, kuwa ni moja ya matukio inayojivunia kampuni hiyo.

Hayo  aliyasema jana wakati wa uzinduzi wa bohari ya bia ya kampuni  hiyo, iiyopo ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha zana za kilimo (ZZK), Iyunga Jijini Mbeya.

Gannon alisema kuwa, kampuni hiyo itaendelea kujitambulisha zaidi kupitia michezo mingine na matukio na kwamba uwepo wa bohari hiyo katika mkoa wa Mbeya, utasaidia vijana wengi kupata ajira za moja kwa moja na zile ambazo si za moja kwa moja.

Alisema wameamua kuwekeza katika mkoa wa Mbeya kiasi cha Shilingi Milioni 500 na kwamba wana imani ya kuleta ushindani na makampuni mengine.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, alsema kuwa serikali inatarajia kuwa uwepo wa bohari hiyo mkoani Mbeya, utaongeza ajira kwa vijana wa elimu za ngazi zote.

No comments: