Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, December 02, 2014

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MADEREVA

Mabasi

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

 SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA)


SHIRIKA la Usafiri Dar es Salaam (UDA) linawatangazia Watanzania wote hususan wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwamba linahitaji kuajiri madereva  kwa ajili ya kuendesha mabasi yake hapa jijini.

 
SIFA ZA WAOMBAJI

Waombaji wa kazi ya udereva wanatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 30-55, ujuzi wa udereva wa mabasi kutoka katika vyuo vya VETA, NIT, au chuo kingine kinachotambulika na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi nchini (NECTA). Pia wanapaswa kuwa na leseni ya udereva daraja C Kavu (Class C Plain) na daraja C1(Class C1) , rekodi nzuri ya utendaji na afya njema.

 

NAMNA YA KUOMBA

Waombaji wote walete barua zao za maombi wakiambatanisha na barua za udhamini, walete barua hizo kwa mkono katika Ofisi ya Afisa Rasilimali watu na Utawala, Makao Makuu ya UDA, KAMATA COMPLEX, mahali zilipokuwa ofisi za mabasi ya SCANDINAVIA.

 

Wanawake wanye sifa wanahimizwa zaidi.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA 255222127421,
0766777754, 0766777753 ,0754776700, 0715776500,0712000037 au wasiliana kwa
barua pepe info@uda.co.tz, uda@umojainvestments.com au kwa
sanduku la posta


Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA)

S.L.P 872, Dar Es Salaam,Tanzania

LIMETOLEWA NA OFISI YA MAHUSIANO YA UMMA UDA

No comments: