Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, December 03, 2014

Tanzania nchi ya 119 kwa rushwa duniani kati ya nchi 174

Tanzania imekuwa nchi ya 119 kwa rushwa duniani kati ya 174 ikifuatiwa na Msumbiji, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Tansparency International.


*Kenya ya 145,
*Uganda 142.

"Kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda imefanya vyema katika kupambana na rushwa ikishikilia nafasi ya 55, ikifuatiwa na Tanzania katika nafasi ya 119, na Uganda ni ya tatu katika nafasi ya 142. Kenya ni ya nne katika nafasi ya 145 na Burundi inashika mkia katika jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 159."

====

Transparency International yasema rushwa ni tatizo kwa wote:


Katika ripoti yake ya leo (03.12.2014) shirika hilo lilisema rushwa inaonekana kukithiri Uturuki na China na limetaka kuwepo ushirikiano wa karibu wa kimataifa kuangamiza kabisa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Katika ripoti yake shirika la Transparency International hilo lenye makao yake Berlin Ujerumani lilisema rushwa ni tatizo kwa uchumi na kuna umuhimu wa taasisi kubwa za fedha katika Umoja wa Ulaya na Marekani kufanya kazi pamoja na nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kuwakomesha mafisadi wasikwepe mkono wa sheria.
Katika faharasa ya 20 inayoonyesha viwango vya rushwa katika mataifa 175, China imepata alama 36 kati ya 100, Uturuki imepata 45 na Angola 19, zikiwa nchi ambazo zimeanguka kwa alama kati ya 4 na 5, licha ya uchumi wao kukua kwa wastani wa asilimia 4 katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Transparency International hutoa alama 100 kwa nchi ambayo haina visa vya rushwa na sufuri kwa nchi ambayo rushwa imeshamiri.

Kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda imefanya vyema katika kupambana na rushwa ikishikilia nafasi ya 55, ikifuatiwa na Tanzania katika nafasi ya 119, na Uganda ni ya tatu katika nafasi ya 142. Kenya ni ya nne katika nafasi ya 145 na Burundi inashika mkia katika jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 159.

Zaidi ya theluthi mbili kati ya nchi 175 katika faharasa hiyo zimepata pointi chini ya 50 huku Somalia, Korea Kaskazini, Sudan, Afghansitan na Sudan Kusini kwa mara nyingine tena zikishika nafasi za chini.
Mkurugenzi wa Transparency International katika mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara, Chantal Uwimana, alisema, "Vipindi vya mizozo huchochea rushwa, kuyumba kwa hali ya kisiasa na kukosekana uthabiti kwa sababu mifumo hudhoofika au wale wanaotakiwa kuisimamia mifumo hii wanapoteza muelekeo.Si jambo la kushangaza kwamba Sudan Kusini na Somalia ambazo zimekabiliwa na vita kwa muda mrefu zinaonekana kuwa na vitendo vya rushwa iliyokithiri."
Denmark ni mfano wa kuigwa
Nchi iliyofanya vizuri kabisa na kushika nafasfi ya kwanza ni Denmark ikijipatia pointi 92, ikifuatiwa na New Zealand, Finland, Sweden na Norway, zote kwa mara nyingine tena zikiwa katika tabaka la nchi tano za kwanza aktika faharasa ya rushwa.


Faharasa kuhusu rushwa ya mwaka 2014

Ukraine ilipata pointi 26 na kubakia kuwa nchi inayoongoza kwa kiwango kikubwa cha rushwa barani Ulaya. Italia,Ugiriki na Romania kwa pamoja zimafanya vibaya miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zikiwa na pointi 43.
Mwenyekiti wa Transparency International, Jos¨¦ Ugaz alisema maafisa mafisadi huficha mali walizozipata kwa njia isiyo halali na kuzificha katika maeneo salama kupitia kampuni. Ugaz aidha amesema ufisadi mkubwa katika nchi zenye uchumi mkubwa haukandamizi tu haki za binadamu kwa watu masikini, bali pia husababisha matatizo ya utawala na uthabiti.
Ripoti hiyo ilizitaka nchi zinazoshika mkia katika orodha iliyochapishwa zichukue hatua madhubuti za makusudi kupambana na rushwa kwa masilahi ya umma. Ugaz aliyataka mataifa yanayoshika nafasi za juu katika faharasa hiyo yasieneze vitendo vya ufisadi katika nchi ambazo hazijaendelea.
Shirika la Transparency International liliuhimiza Umoja wa Ulaya, Marekani na kundi la G20 la mataifa yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi, kuiga mfano wa Denmark na kuanzisha daftari la umma linalojumuisha tarifa muhimu za wamiliki kwa kampuni zote zilizoshirikishwa.

Ripoti kuhusu viwango vya ufisadi duniani yatolewa

Afghanistan, Korea ya Kaskazini na Somalia ndio nchi zinazoonekana kuwa na ufisadi mkubwa zaidi ulimwenguni, wakati Denmark na New Zealand zikiwa ndio nchi zenye zaidi.


Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka iliyotolewa leo na Shirika la Kimataifa la kupambana na Ufisadi la Transparency International. Shirika hilo limesema kuwa kutokana na ukweli kwamba zaidi ya thuluthi mbili ya nchi zinaghubikwa na ufisadi, ni hali ambayo itaathiri ukuaji wa uchumi na kukwamisha vita dhidi ya umaskini na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Transparency International ¨C TI lenye makao yake mjini Berlin, kuwa karibu asilimia 70 ya mataifa yote ulimwenguni yanafikiriwa kukabiliwa na ¡°tatizo kubwa¡± la ufisadi katika sekta ya umma, na hakuna moja kati ya nchi 177 zilizofanyiwa utafiti mwaka huu iliyopata alama nzuri. Orodha ya kila mwaka ya TI ndicho kipimo kinachotumiwa zaidi kuangazia ufisadi katika vyama vya kisiasa, polisi, mifumo ya mahakama na utumishi wa umma, janga ambalo lina athari juu ya hatima ya maendeleo ya nchi na vita dhidi ya umaskini.

Maskini ndio wanaoumia

Wananchi wakiandamana Nigeria kuhusiana na kuondolewa ruzuku kwa bidhaa za mafuta

¡°Ufisadi unawaumiza sana watu maskini¡± amesema Mtafiti mkuu Finn Heinrich, na kuendelea kueleza kuwa hicho ndicho unachokiona wakati unapoziangalia nchi zilizoshika mkia kwenye orodha. Ndani ya nchi hizo, amesema mtafiti huyo, watu maskini ndio wanaoumia sana, na nchi hizo kamwe haitaweza kuondoka katika janga la umaskini ikiwa hazitapambana na ufisadi.

Miongoni mwa nchi ambazo zimeshuka zaidi kwenye Ripoti ya Orodha ya Ufisadi mwaka wa 2013 ni Syria inayokabiliwa na vita, pamoja na Libya na Mali, ambazo pia zimekabiliwa na migogoro ya kijeshi katika miaka ya karibuni.

Miongoni mwa nchi ¡°zilizopiga hatua nzuri¡±, ijapokuwa kutoka kiwango cha chini, ni Myanmar, ambako utawala wa kijeshi umefungua milango ya mchakato wa demokrasia na huku ikineemeka na nafasi kubwa ya uwekezaji, na kugeukia zaidi sheria za uwazi na uwajibikaji. Heinrich anasema hiyo ndiyo njia pekee nchi zinaweza kuepuka ¡°laana ya raslimali¡± ambako raslimali hupatikana tu kwa walio wachache na wenye uwezo.

Nigeria, na nchi nyingine zenye utajiri wa mafuta bila shaka ni mifano mizuri.

Nchi zenye migogoro zinaongoza kwa rushwa

"Ugiriki imesifiwa kwa kupunguza ufisadi"

Nchi zilizoorodheshwa katika nafasi za mwisho ni pamoja na Iraq, Syria, Libya, Sudan na Sudan Kusini, Chad, Guinea ya Ikweta, Guinea Bissau, Haiti, na Yemen. Nazo nchi zilizofanya vyema ni Denmark, New Zealand, Luxembourg, Canada, Australia, Uholanzi, Uswisi, Singapore, Norway, Sweden na Dinland.

Rwanda iliyo katika nafasi ya 49 ulimwenguni imetajwa kufanya vyema katika eneo la Afrika Mashariki ikifuatwa na Tanzania iliyo katika nafasi ya 111, Kenya katika nafasi ya 136, Uganda inayokuja katika nafasi ya 140, na Burundi iliyo kwenye nafasi ya 157. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inajikuta katika nafasi ya 154 kwenye orodha hiyo.

Heinrich amesema ufisadi unahusishwa na nchi zinazosambaratika kutokana na migogoro na ambazo serikali haziendeshwi kikamilifu na hivyo watu ni lazima watumie kila mbinu kuendesha harakati zao, kupata huduma, kupata chakula na kuishi.

Mtafiti huyo amesema Afghanistan ambako majeshi mengi ya magharibi yanayoongozwa NATO yanaondoka mwaka ujao baada ya kuwa nchini humo kwa zaidi ya mwongo mmoja, ni ¡°hadithi ya kutisha¡±.
Kwa sababu hawajaona mabadiliko yoyote makubwa. Nchi za magharibi zinawekeza kiasi kikubwa siyo tu katika masuala ya usalama lakini pia zinajaribu kurejesha mkondo wa sheria, lakini bado utafiti wa miaka ya karibuni unaonyesha kuwa idadi ya watu wanaotoa hongo bado ni ya juu kabisa ulimwenguni.


Chanzo: DW

No comments: