Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, January 21, 2015

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA YATOA 162ML MIKOPO VIKUNDI 50
Na. FESTO MWALYEGO - MBEYA

MKUU wa wilaya ya mbeya prof. Norman sigalla, amekabidhi hundi ya shilingi 162 Mil,  kwa ajili ya mikopo ya vikundi 50 vya wanawake na vijana vya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya 

Hundi hiyo aliikabidhi Januari 16, 2015.

Katika hotuba yake prof. sigalla, aliwapongeza mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya, mkurugenzi mtendaji  na wakuu wa idara na madiwani, kwa jitihada za makusudi kuhakikisha vikundi vya wanawake na vijana wanapata mikopo ya kuwawezesha kukuza mitaji yao na kuongeza kipato kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Vongozi wa vikundi waliohudhuria katika hafla hiyo kwa  kufanyiwa utafiti na kuaminiwa, aliwasihi kutumia mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kupanua miradi ya kilimo,ufugaji na biashara ndogondogo na kurejesha kwa wakati ili wengine wanaohitaji wapate fursa hiyo.

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Marieta Mlozi, alibainisha kuwa mkopo huo umeongezeka kutoka shilingi 106 Mil, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 162mil 2014/2015.

Alisema kuwa mkopo shilingi 99ml ni kwa ajili ya wanawake na riba ya 12%  na 63mil kwa vijana riba ya 15% na ulitolewa kwa kata 15 za halmashauri ya wilaya ya Mbeya  kwa kipindi cha mwaka mmoja unaotarajiwa kurejeshwa Januari  2016.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya,  Andason Kabenga, aliwakumbusha viongozi wa vikundi kuwa serikali inayoongozwa na CCM inawathamini na kutekeleza ilani yake kwa kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapa mikopo yenye masharti nafuu.

Hata hivyo mh  Kabenga ambaye pia ni diwani wa kata ya Iwiji aliwasisitiza kuendelea kuwa na imani na viongozi wao kwa kuwa wameendelea kuwawakilisha vizuri na kuwafikishia huduma muhimu katika vijiji na kata za halmashauri ya wilaya ya Mbeya. 

No comments: