Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, January 01, 2015

KUHUSU ACT KUFUKUZA VIONGOZI WAKE, PROF. KITILA MKUBWA ANASEMA


Hizo ni mbwembwe za kupokea mwaka mpya. Na ukiona jambo la ACT linachangamkiwa na Saed Kubenea ujue kuna mambo. Taarifa kamili ya chama hii hapa:

Siku ya Jumatano tarehe 31 Desemba 2014 Mwenyekiti wa Muda wa Taifa wa ACT-Tanzania Ndugu Kadawi Lucas Limbu aliitisha mkutano wa waandishi wa habari. Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, alitangaza kuwavua uanachama Katibu Mkuu wa Muda wa ACT Tanzania ndugu Samson Mwigamba pamoja na wanachama wengine kadhaa. Ndugu Limbu alieleza kwamba maamuzi aliyoyatangaza yalifanywa na Kikao cha Kamati Kuu ya ACT Tanzania ambacho alidai kilifanyika tarehe 30 Desemba 2014. Kupitia taarifa hii napenda kufafanua kuwa:
 
1.     Hakuna Kikao cha Kamati Kuu kilichoketi katika tarehe iliyotajwa na Ndugu Kadawi Lucas Limbu. Kikao cha Kamati Kuu kimepangwa kufanyika siku ya Jumatatu tarehe 5 Januari 2015 Jijini Dar es Salaam, kama kilivyoamuliwa na Kikao cha Sekratariati cha Tarehe 23 Desemba 2014, ambacho ndicho chenye jukumu la kikatiba la kuandaa ajenda za vikao vya Kamati Kuu kwa Mujibu wa Katiba ya ACT-Tanzania (Ibara 37 q (iii)
2.     Maamuzi yaliyotangazwa na Ndugu Kadawi Limbu ni batili kwa mujibu wa Katiba ya ACT Tanzania na Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania
3.     Ndugu Samson Mwigamba na viongozi wengine wa muda wa ACT-Tanzania waanaendelea na nafasi zao hadi pale uchaguzi utakapofanyika kwa ratiba itakayopangwa na Kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 5 Januari 2015 au itakavyoamuliwa vinginevyo na vikao halali vya chama.
 
Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania
Thomas Matatizo (LLB)
Mwanasheria wa ACT-Tanzania.
31 Desemba 2014 
NIMEIOTOA MAHALA HIYO.
 

No comments: