Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, January 01, 2015

MBEYA;MWAKABWANGA AJENGA KIVUKO NA VISIMA MBARALI

KAMPUNI ya usafirishaji ya Usangu Logstics Ltd,(Mwakabwangas), imejenga kivuko kinachounganisha Tarafa za Ilongo na Rujewa, katika wilaya ya Mbarali mkoani hapa.

Akizungumza na kikosi kazi cha blog hii ya
wilayani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ibrahim Ismail, alisema kuwa kampuni yake ilifikia uamuzi huo baada ya mwaka jana kutembelea eneo hilo na kumuona Bibi kizee ambaye alikuwa akivuka kwa miguu ndani ya maji huku akihitaji msaada.

Alisema hali hiyo ilimgusa na kuamua kushirikisha uongozi wa kampuni yake na kuamua kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa kivuko hicho kisha kukitengeneza Jijini Dar es Salaama na kupeleka wataalam wengine katika eneo hilo kwa ajili ya kukifunga na sasa kimeanza kutumika.

“Tangu dunia kuwepo, hakujakuwepo kivuko, lakini kivuko hiki kwa sasa kimekuwa mkombozi kwa wananachi na ni sadaka yangu kwa Mungu kwa ajili ya kuhudumia watu hasa wajawazito na wazee. Kina uwezo wa tani 25 na sahani ya kukalia, ina uwezo wa kubeba watu nane na kimegharimu Shilingi Milioni 35” alisema Ibrahim.

Mbali na kivuko hicho, alisema tayari ameanza ujenzi mwingine wa kivuko cha mto Barali kitakachokuwa na urefu wa mita 100, kitakacho gharimu kiasi cha Shlingi Milioni 35.

Sambamba na vivuko hivyo, alitembelea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbarali mwanzoni mwa wiki hii na kuwapa pole kwa kuwapatia sabuni na kwamba alichokigundua ni kwamba kuna uhaba wa vitanda vya wagonjwa.

Kampuni ya (Mwakabwangas), kwa kutambua tatizo la maji safi katika wilaya hiyo, imechimba visima vya kisasa katika maeneo ya Isisi, Utengule Usangu ambako ndiyo chimbuko la kampuni hiyo na Ilongo, vinavyogharimu Shilingi Milioni 80 kwa kila kimoja.

No comments: