Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, January 08, 2015

MTOTO MCHANGA ATELEKEZWA HOSPITALINI, WALINZI WALIDHANI (MWANGA)


Na Daniel Limbe, Chato

WAKATI Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 11 zinazoongoza kwa vifo vya watoto wachanga duniani, mwanamke ambaye hajafahamika jina wala makazi yake, amemtelekeza mtoto mchanga nje ya uzio wa hospitali ya wilaya ya Chato mkoani Geita kisha kutokomea kusikojulikana.

Mtoto huyo anakadiliwa kuwa na siku tatu tangu alipozaliwa kabla ya kutupwa usiku wa manane kwenye majani yaliyopo eneo hilo.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya chato.Dk Pius Buchukundi, alisema tukio hilo lilibainika baada ya walinzi wa hospitali hiyo kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia kwa muda mrefu pasipo kuonekana mzazi wake.

"Mtoto huyo alilia sana kuanzia majira ya saa nane usiku...baada ya walinzi kusikia hivyo waliogopa na kuhisi wachawi (Wanga),  lakini ilipofika majira ya saa 12 asubuhi ya desemba 14, 2014, waliamua kwenda kujilidhisha".alisema Dk. Buchukundi.


"Walivyobaini kuwa ni mtoto mchanga,walimwamsha mmoja wa madaktari wetu (Dk.Alexandar Mpondaguzi) ambaye alifika eneo hilo na kuwataka wananchi waliojitokeza eneo hilo kumchukua mtoto huyo ambaye alikuwa uchi na kumpeleka kituo cha polisi kabla ya kuanza kumpatia matibabu".

Alisema mtoto huyo anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya awali.
Mtuhumiwa anatafutwa kwa jalada la kipolisi namba CHT/RB/1906/2014 na kwamba taarifa za awali zinaeleza mzazi huyo hajapatikana.

Mkuu wa polisi wilaya ya chato,Alex Mukama,alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa uchunguzi unaendelea ili kumbaini mwanamke huyo aliyehusika na ukatiri huo na kuiomba jamii kutoa ushirikiano utakaoweza kusaidia kumkamata mtuhumiwa huyo.

Afisa ustawi wa jamii hospitali ya wilaya ya Chato,Leonia Mkingule,alisema jitihada za kutafuta michango kutoka kwa wasamaria wema zinafanyika ili kumsafirisha mtoto huyo kwaajili ya malezi kwenye kituo cha kulelea watoto.

"Hivi sasa tunakusanya michango ili tumsafirishe mpaka Bukoba kwenye kituo cha kulelea watoto wadogo cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kaskazini magharibi...na tunaendelea na mawasiliano na wahusika" 

"Mtoto ni mchanga sana na hatuwezi sisi kumlea...kwani anahitaji uangalizi wa hali ya juu...maana hata kitovu chake ndo kimeanza kusinyaa...ila tunashukuru Mungu bado yupo hai na anaendelea vizuri"alisema Mkingule.

Mmoja ya wajawazito waliozungumza na gazeti hili,Stella Emmanuel (32) ameiomba serikali kutunga sheria kali dhidi ya wanawake wanaowatelekeza watoto wao kwa makusudi, kwa madai isipokuwa hivyo kuna hatari kubwa ya kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga na wale wa mitaani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Mama Ye! takribani watoto wachanga 39,000 wa Tanzania hufariki kila mwaka kutokana na masuala ya uzazi na wengine 22,000 huzaliwa wafu.

No comments: