Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, July 04, 2016

Chama kipya cha walimu chatema cheche kuhusu Elimu

Na Gordon Kalulunga.

CHAMA kipya cha Kutetea Haki na Masilahi ya Walimu Tanzania

(CHAKAMWATA), kimewasilisha serikalini hoja na madai yapatayo ishirini (20) ya walimu nchi nzima tangu kiliposajiliwa Machi, 18, 2015.


Akizungumza na
mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com
mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa chama hicho, Mwalimu Meshack Kapange alisema kuwa madai hayo ya walimu yaliyowasilishwa  serikalini kupitia Waraka wenye kumbu kumbu namba CMT.012/016/01/144 wa April, 26 mwaka huu, yanahusu hoja halisi za walimu kuhusu kero sugu zinazowakabili na kupelekea kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.


“CHAKAMWATA kimeziwasilisha hoja zake serikalini kupitia ofisi ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, na Makatibu Wakuu wa Wizara za Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofsi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Katiba na
Sheria na Wizara ya Fedha na Mipango” alisema Kapange.


Mbali na taasisi hizo, pia madai yao ameyaeleza kuwa wameyapeleka
kwenye taasisi, Idara na Mamlaka za serikali kama, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Regulatory Authority – SSRA), Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania na kwa Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Idara ya Utumishi wa Walimu (TSD).


Mwalimu Kapange amezitaja hoja ambazo chama chao kimeziwasilisha
serikalini kuwa ni pamoja na kuulalalamikia mfumo wa ajira za walimu nchini ambapo Wizara zipatazo tano na Idara moja zinahusika  kama waajiri wa walimu, wizara hizo.


Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na

Mafunzo ya Ufundi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serkali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma Idara huru ya Utumishi wa Walimu (TSD), Wizara ya Fedha na mpango na Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu.


Alisema wizara zinazoongoza kuzalisha kero na malalamiko ya walimu
nchini ni Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutokana na nyaraka kandamizi inazoziandika bila kuwashirikisha walimu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serkali za Mitaa (TAMISEMI) na Tume ya Utumishi wa Umma Idara huru ya Utumishi wa Walimu (TSD) zinashirikiana kuzalisha kero na malalamiko ya walimu katika masuala yote yahusuyo madara na madeni mbalimbali ya walimu ambapo katika waraka wa CHAKAMWATA kwa serikali TSD imetajwa kuwa ni kero inayojitegemea.


Kero ya tatu imetajwa kuwa ni sheria namba 8/2008 kuhusu kanuni mpya
ya kukokotoa malipo ya pensheni na mafao ya kustaafu kwa wafanyakazi wote wa Umma na wa sekta binafsi ambapo imabainishwa kuwa sheria pamoja na kanuni hiyo ni kandamizi na zinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 kwa ujumla wake na inapunguza malipo ya pensheni na mafao ya kustaafu kati ya asilimia 6.9 mpaka asilimia 62.46 ukilinganisha na kanuni iliyopo sasa.


“Hoja ya nne ni Kanuni ya kodi ya mapato inayoitwa Pay As You Earn
(PAYE).amesema tatizo siyo asilimia kama ilivyotajwa na Mheshimiwa Rais John Magufuli kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani mjini Dododma, bali tatizo ni Kanuni yenyewe. Amesema kwa mujibu wa kanuni hiyo, alichokitaja Rais ni puunguzo la shilingi elfu tano mpaka elfu saba tu, wafanyakazi bado wanaendelea kulipa kodi mpaka kufikia asilimia 29 ya mishahara yao kwa mwezi.”


“Hoja yetu ya tano ni walimu na wafanyakazi wote nchini kubaguliwa
katika sera za Mkakati wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Tanzania (MKUKUTA) kiuchumi wafanyakazi wako chini zaidi kuliko wafanyabiashara wadogo lakini wafanyabiashara wadogo wanalipa kodi ya mapato iliyo ndogo zaidi na wafanyakazi wanalipa kodi ya mapato iliyo kubwa zaidi kwa mwaka kwa kutumia kanuni ya kodi ya zuio (withholding Tax) kutoka katika mishahara midogo zaidi kuliko mapato ya wafanyabiashara wadogo.” Alisema Kapange


Katika mtiririko wa hoja zao, wamezitaja pia hoja ya sita na hoja ya

saba kuwa ni nyaraka kandamizi zinazoandikwa na Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo walimu wote wanaojiendelea kielimu wanakandamizwa kimasilahi. Saba inawahusu walimu wa shule za sekondari wanaofundisha masomo ya ufundi wanavyopata kero wanapojiendeleza kielimu katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya Juu za ufundi kama vile Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya au Chuo cha Ufundi cha Arusha, ambapo serikali inakataa kuzitambua shahada (Degree) hizo katika miundo ya ualimu kwa kuwa hakuna chuo kikuu nchini kinachotoa shahada ya ufundi na ualimu.


Hoja ya nane inahusu shida na changamoto mbalimbali wanazozipata
walimu wasioona na wanafundisha katika shule za kawaida za wanafunzi wanaoona kwa kuwa wanalazimika kuajiri wasaidizi wa kuwasaidia katika kukutafsiri mawasiliano ya maandishi kutoka maandishi ya nukta nundu kwenda maandishi ya kawaida ili wanafunzi waweze kunakili na matatizo mengine mengi.


Hoja ya tisa ni ubaguzi wa miundo kati ya walimu wenye viwango sawa
vya elimu lakini wanaofundisha katika vyuo vya ualimu wanalipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko walimu wanaofundisha katika shule za msingi na shule za sekondari. Hoja ya kumi inahusu upendeleo unaofanywa na idara ya utumishi wa walimu kwa kushirikiana na wakururgenzi wa halmashauri katika upandishaji madaraja walimu ambapo Mwalimu Meshack Kapange amesema wapo walimu ambao hawajapandishwa madaraja kwa muda wa zaidi ya miaka nane sasa.


“Hoja ya kumi na nne inahusu malalamiko ya walimu dhidi ya Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) kukata asilimia 2 kwenye mishahara ya walimu bila ridhaa ya walimu, Usiri kuhusu mapato na matumizi ya fedha zinazokatwa kwenye mishahara ya walimu, usiri kuhusu mapato na matumizi ya fedha zinazotokana na vitega uchumi mbalimbali na maghorofa ya CWT nchi nzima, usiri kuhusu mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na wahisani wa nje ya nchi kama vile chama cha walimu cha Denmark (The Danish Union of Teachers in Tanzania)” alisema Katibu huyo.

No comments: