Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, July 19, 2016

IJUE PAROLE

Parole ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka minne na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum baada ya kukidhi vigezo vifuatavyo:
1. Awe ametumikia theluthi (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwenendo wa kurekebika kurudi katika jamii kumalizia sehemu ya kifungo chake kwa masharti maalum. Masharti hayo ni:
a. Kuwa chini ya uangalizi maalum kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka atakapomaliza kifungo chake.
b. Kuzingatia masharti ya Parole anayopewa kikamilifu
c. Kuwa raia mwema na kuishi kwa kujipatia kipato halali katika jamii.
ii).    Awe ameonesha kujutia kosa, kurekebika tabia na kuonesha mwenendo mzuri gerezani.
d. Mamlaka husika kujiridhisha kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.
Parole ni moja kati ya adhabu mbadala na imeonesha mafanikio makubwa katika nchi nyingi duniani.  Utaratibu huu ni wa kipekee kwa kuwa unawagusa wafungwa wa vifungo virefu ambao ndio wengi waliopo magerezani. Aidha, ni utaratibu unaoshirikisha jamii katika urekebishaji kwa kuzingatia usalama wa jamii na dhana kwamba uhalifu ni zao katika jamii.


MUUNDO WA BODI ZA PAROLE
Kwa mujibu wa Sheria ya Bodi za Parole (Cap 400 R.E 2002) kifungu cha 3(2)(a-d) na 3(4-9) Bodi zifuatazo ziliundwa ili kuhakikisha kuwa  Sheria ya Parole inatekelezeka hapa nchini.

3.1    Bodi ya Taifa ya Parole:

Bodi hii inaundwa na Wajumbe wafuatao:-
a)    Mwenyekiti wa Bodi ambaye huteuliwa na Mheshimiwa Rais.

b)    Wajumbe wawili ambao huteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

c)    Wajumbe sita ambao huingia kwenye Bodi kutokana na nyadhifa zao.

Wajumbe hao ni:-
i).    Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) au Mwakilishi wake
ii).    Mganga Mkuu wa Serikali
iii).    Kamishna wa Ustawi wa Jamii
iv).    Afisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais
v).    Mkuu wa Jeshi la Polisi au mwakilishi wake
vi).    Mkuu wa Jeshi la Magereza ambaye ndiye Katibu wa BodiUAMUZI BODI ZA PAROLE UNAVYOFANYIKA
Kimsingi mfungwa anapoingia gerezani kwa mara ya kwanza hujulishwa kuhusu haki zake ikiwemo haki ya kuingizwa kwenye mpango wa Parole kama ana sifa kulingana na kosa lake na muda wa kifungo chake gerezani.  Mfungwa mwenye sifa ya kuingizwa kwenye mchakato wa Parole anapotimiza 1/3 ya kifungo chake, Afisa Parole hukusanya taarifa mbalimbali zinazomuwezesha kujadiliwa katika Bodi za Parole;  Taarifa hizo ni maoni kutoka kwa wazazi/ndugu zake, maoni ya mwathirika wa uhalifu, nakala ya hukumu, hati ya kifungo, maoni kutoka uongozi wa kijiji anachotarajia kwenda kuishi na maoni/taarifa kutoka kituo cha polisi kilichomkamata na pia matokeo ya uchunguzi wa alama zake za vidole kuhusu kumbukumbu zake za uhalifu.  Taarifa hizi zote huwa ni kwa ajili ya kudumisha usalama wa jamii na wa mfungwa mwenyewe anufaikapo kwa Parole.

Baada ya Taarifa hizi zote kukamilika kila mfungwa anayependekezwa kunufaika na Parole hufunguliwa jalada (Prison Form 64) kwa ajili ya kutunza kumbukumbu zake pamoja na taarifa za tabia na mwenendo wa mfungwa. Mchakato wa kumjadili mfungwa huanzia katika Kamati za Urekebishaji ya Gereza. Kamati hiyo hupitia taarifa hizo na kutoa maoni na mapendekezo kwenda Bodi ya Parole ya Mkoa.  Bodi ya Parole ya Mkoa hupitia maoni na mapendekezo hayo na baada ya uchambuzi wa kina, hutoa mapendekezo yake kwa Bodi ya Taifa ya Parole kupitia kwa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole.
Sekretarieti ya Taifa ya Parole ina jukumu la kuratibu shughuli za Bodi. Hivyo hupokea taarifa za wafungwa waliopendekezwa au kutopendekezwa kunufaika na Parole kutoka katika Bodi za mikoa. Huchambua taarifa hizo na kuandaa taarifa ya kila mfungwa kwa ajili kujadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole. Bodi hiyo kwa kutumia taaluma mbalimbali walizonazo wajumbe wake na nyadhifa zao hufanya uchambuzi wa kina wa mawasilisho hayo na kutoa uamuzi mfungwa anufaike au asinufaike na Parole. Uamuzi wa Bodi ya Taifa ya Parole huwasilishwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa Kifungu cha 6(4) cha Sheria ya Bodi za Parole Na 25 ya mwaka 1994 (Sura ya 400 R. E 2002). Mheshimiwa Waziri hupitia taarifa za kila mfungwa na kutoa uamuzi wa mwisho wa kukubaliwa au kukataliwa kunufaika kwa mpango wa parole. Uamuzi huo huwasilishwa kwa Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza.

No comments: