Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, July 25, 2016

Kikwete alikuwa kama kondoo katikati ya Mbwa Mwitu

NA GORDON KALULUNGA

JANA Julai 23,2016, Rais wa awamu ya Nne wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete, amemkabidhi Rais wa awamu ya tano, Dkt. John Magufuli nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa mjini Dodoma.

Kutokana na makabidhiano hayo, baadhi ya wana CCM na watanzania
wanaamini kuwa kutatokea mabadiliko makubwa ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.

Mwenendo wa kilipokuwa kimefikia, baadhi ya wanachama walikata tamaa
kupata nafasi za ajira ndani ya chama hicho kwasababu walikuwa wanaamini kuwa nafasi nyingi hasa za ukatibu zilikuwa zikitolewa kwa misingi ya dini na kujuana, kibaya zaidi hata waliozipata baadhi yao hawamudu kazi.

Wakati wengine wakifurahi kukabidhiwa nafasi hiyo Dkt. Magufuli,

baadhi mioyo yao imejaa hofu ya kutumbuliwa huku taswira za vivuli vya waliowapa ajira zikiwajilia kila uchwapo.

Baadhi ya watumishi wa chama hicho na baadhi ya watumishi wa serikali,
wamefanya sherehe na baadhi mioyo yao inabubujikwa na machozi kwa Dkt.Kikwete kung'atuka katika nafasi hiyo kwasababu wanaona wingu zito la manyunyu ya mvua halisi za kuisimamia serikali zikiwaendea.

Wana ndoa wakiishi kwa muda mrefu huwa wanafanana kwa sura au tabia.
 

 Ninaamini kuwa hata kwa upande wa baadhi ya wanachama wa CCM, mapaji ya nyuso zao hayana furaha, maana tayari walizoea raha za uongozi wa kutoguswa chini ya Dkt. Jakaya Kikwete.

Kuna baadhi ya wananchi wanasema Rais mstaafu, Jakaya Kikwete

hakufanya kitu katika utawala wake, wanasema hayo kwasababu ni wepesi wa kusahau historia.

Dkt. Kikwete alitoa fursa kwa wananchi wa Tanzania kupendana na

kuheshimiana huku akiwaweka wanachama wa chama chake katika umoja ambao uliparaganyika wakati wa kuelekea katika uchaguzi Mkuu 2015 na sasa umeanza kurejea kutokana na kutojua kesho yao chini ya Dkt. Magufuli.

Wanafanya kila namna kujipendekeza ili waonekane ni wema. Baadhi
wakitaka vyeo na baadhi wakihofia kutoka katika nafasi zao.

Nawasifu makundi yote mawili yaani ya wanaojipendekeza kwa kutaka vyeo
na wale wanaojipendekeza ili kubaki kwenye nafasi zao, maana fursa ikionekana ni kuiendea na wala siyo kuisubiri ikufikie (ila kesho yako ni woga kukutawala).

Kuna siku huku Nyikani mhamasishaji (Motivational speaker) alitoa

mfukoni noti za shilingi elfu kumi kumi zilizokuwa na jumla ya shilingi laki moja, akauliza, "ni nani miongoni mwenu anataka nimpe hii laki moja?"

Watu wengi waliokuwa mle ukumbini walinyosha mikono, kila mmoja
alikuwa akisema mimi! Mimi!. Nikaanza kushangaa ni nani atakuwa na bahati ya kupewa ile pesa kati ya mamia ya watu waliohudhuria ile semina.

Pia nikajiuliza kwa nini (ambapo bila shaka na baadhi ya wahudhuriaji
wengine nao walijiuliza) atoe kitita cha shilingi laki moja kirahisi rahisi hivyo.

Wakati watu wakiendelea kupiga kelele kusema nipe mimi, nipe mimi huku
wamenyoosha vidole vyao juu, kutokea nyuma akaibuka msichana mdogo mwenye umri kama miaka 12 hivi, akaenda mbele kule aliko yule speaker akapanda stejini na kuchukua ile laki moja kutoka mkononi mwa yule mhamasishaji.

"Safi sana, msichana! Umefanya vema," alisema yule mhamasishaji.

"Wengi wetu tunapenda kukaa tu na kusubiri mambo mazuri yaje yenyewe.


Hii haitaweza kuwasaidia hata kidogo, unatakiwa kuinuka na kutafuta mafanikio. Mafanikio hayawezi kuja kama umekaa tu, lakini sidhani kujipendekeza kama ni njia nzuri (Tumia kama inakufaa).

Suala hili la kujibidiisha, Dkt. Kikwete, amekuwa muhubiri mzuri.


Aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM Taifa, Mzee Yusuph Makamba mwaka 2012
mjini Dodoma kwenye kikao cha NEC, aliwahi kusema kuwa waswahili wanasema ukimsifia mtu wakati yupo sawa na kumtusi wakati hayupo.

Aliyasema hayo alipokuwa akimuombea kura za uenyekiti Dk. Jakaya
Kikwete baada ya kuwepo taarifa za kupiga kura za Maluani huku akisema kuwa aliwahi kuonekana mbaya kwa kusema ukweli.

Binafsi sijachukia Dkt. Kikwete kuondoka katika nafasi ya Uenyekiti wa
CCM taifa kabla ya mwaka 2017, bali nafurahi kwa alama njema alizoziacha mioyoni mwa miongoni mwa baadhi ya Watanzania huku akiwaamini sana watendaji wake ambao walikuwa wakitumia vibaya nafasi zao.

Kazi za utumishi ni utume sawa na kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa
kheri Jakaya Kikwete, karibu sana Nyikani.

No comments: