Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Saturday, July 23, 2016

Magufuli: Watoa rushwa kwenye chaguzi za CCM wakiahidi kutoshwa

DODOMA TANZANIA.

RAIS John Magufuli wa Tanzania,  amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amesema hatowavumilia watoa rushwa ndani ya chama hicho.

Hayo ameyasema mjini Dodoma Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Dkt. Jakaya Kikwete.

Amesema imefikia hatua watu wenye karama za uongozi wanakosa nafasi za kuchaguliwa kwasababu ya kutokuwa na fedha za kujenga.

Ameahidi kuwatosa wale wote ambao wataendelea na vitendo hivyo vya rushwa na kwamba ataboresha maslahi ya watendaji wa chama na watumishi wa serikali ambao hawatawatii Viongozi wa chama nao watashughulikiwa.

No comments: