Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, August 14, 2016

AKEKETWA NA BABU YAKE KWA KUTUMIA KIGAE CHA MOTO

Wakati serikali ikipinga mila potofu katika jamii hali imekuwa tofauti katika kijiji cha Mfumbi Kata ya Mfumbi Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya baada ya mwanafunzi wa darasa la pili kukeketwa na babu yake alipokuwa akitafuta kuni msituni.

Kwa mujibu wa wazazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), wamesema kuwa tukio hilo limefanywa na babu yake alipokuwa akitema kwa kushirikiana na mtu mwingine ambaye hajafahamika, kwa kutumia kigae cha Moto.

Baada ya kufanya ukatili huo babu yake na mwenzake wametoweka kusikojulikana na suala hilo linahusishwa na imani za kishirikina maarufu kama nyambuda. Hata hivyo juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wote zinaendelea kwa kushirikiana na Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Mfumbi.

Naibu Katibu mkuu wa MUJATA Wilaya ya Mbarali Bruno Mwaijande amesema kuwa taarifa ya wahalifu ya hao ilifikishwa ofisini kwake baada ya kuletewa taarifa na wasiri ndipo alipoanza kunifanyia kazi na kubaini ukweli wa tukio hilo ingawa amesikitishwa na uongozi wa kijiji kushindwa kuchukua hatua za awali kuweza kuwakamata watuhumiwa.

 Aidha imedaiwa kuwa babu aliyetenda uhalifu huo anaogopwa kwa imani za kishirikina ambapo matukio kadhaa amehusishwa ikiwa ni pamoja na vitendo vya unyambuda.

Mara baada ya kufanyiwa ukatili huo mtoto alirejea nyumbani kwa taabu ndipo wazazi baada ya kugundua walimpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu na sasa ameanza masomo.

Mpaka sasa suala hilo limekuwa tete kutokana na kukosa mtu wa kulisimamia ili wahalifu watiwe nguvuni na kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini.

No comments: