Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Thursday, August 11, 2016

BREAKING NEWS......Serikali yalifunga gazeti la MsetoSERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na Michezo, imelifunga gazeti la MSETO kwa miezi 36 kwa kosa la kugushi nyaraka za serikali.

Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo Nape Nnauye, ametangaza maamuzi hayo leo Dar es Salaam kwa kusema kuwa Serikali imekuwa ikimuonya Mhariri wa gazeti hilo kuacha kuandika habari za uchochezi tangu mwaka 2012 lakini Mhariri hakuweza kufanya hivyo.

Aidha amesema hivi karibuni gazeti hilo limechapisha habari zisizo za ukweli kuhusu Rais Dkt. John Magufuli.

Gazeti MSETO halitatakiwa kuchapishwa mahala popote hata kwa njia ya mitandao (Online publication). 

No comments: