Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, August 10, 2016

Daktari aliyegushi vyeti na kutoroka anaswa

Na Ezekiel Kamanga, Songwe

Moses Jackson Mgala(36)mkazi wa Mbozi Mkoa wa Songwe anashikiliwa na Jeshi la polisi baada ya kutoroka kifungo cha nje cha miaka mitatu.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Mathias Nyange amesema Mgala alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu mapema mwaka huu katika kesi namba CC /220/2016 kwa kosa la kughushi vyeti vya udaktari na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo mahakama ya Wilaya ya Mbozi ilimkuta na hatia na alipaswa kufanya usafi katika Zahanati ya Kijiji cha Magamba Wilaya ya Mbozi.

Huku akitumikia kifungo Mgala alitoroka kifungo na kughushi vyeti tena na kujipatia ajira katika Hospitali teule ya Ifisi Wilaya ya Mbeya.

 Polisi walimkamata mwishoni mwa wiki iliyopita na kumrudisha Songwe kwa mahojiano zaidi.

Kamishina msaidizi wa Polisi Mkoa wa Songwe Mathias Nyange amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani hivi karibuni pindi upelelezi utakapokamilika.

No comments: