Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Monday, August 22, 2016

DC KASESELA AWASWEKA NDANI WALINZI WAWILI WA KAMPUNI YA AMAZON SECURITY KWA KUNYANYASA WANANCHI

 Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, akimweka chini ya ulinzi mlinzi wa kampuni ya Amazon mjini Iringa baada ya kudaiwa kuwanyanyasa wananchi waliokuwa eneo la Hospitali.Ni kama anasema (Pole sana mama, Serikali hii ni ya wanyonge, tupo pamoja)

Na www.mpakani.com

Iringa

JANA majira ya saa 3 na dakika 25 Usiku,  mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alipokea wakina mama 3 wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa walio lazwa hasa kwa wale walio toka mbali. 

Maji hayo yalimwagwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa. 

Mkuu wa wilaya alifika hospitali kujionea mwenyewe hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula hospitali na kumwaga kwa mateke. Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. 

"Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuroweshwa maji." alisema Mh Kasesela.

No comments: