Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, August 31, 2016

JAJI WARIOBA ALIPOCHAMBUA KELELE NA KUZIFANYA SAUTI ZA NYIKANINA GORDON KALULUNGA.

POLE na kazi ndugu yangu Jaji Joseph Sinde Warioba, mtoto wa Kijijini kwetu kata ya Nyamuswa, tarafa ya Ikizu wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Ingekuwa kupitia posta ningekuletea kwa telegram maneno haya, lakini kwasababu ni sauti kutoka hapa Nyikani, hebu isikilize ingawa nitakueleza kwa mtindo wa barua.

Nakupa pole sana na kazi za ujenzi wa taifa, nimearifiwa kuwa katika tume yako ya mabadiliko ya katiba kuna baadhi ya watu wanasema eti mengi uliyoyaandika na wenzako kwenye rasimu ni mawazo yako.

Kuna wengine wanakutetea na kufikia hatua ya kusema tume yako isivunjwe na iendelee mpaka siku ya mwisho.

Lakini inawezekana yote hayo yanakuja kutokana na mawazo uliyoyakusanya mwanzo kuungwa mkono na watu wengi wa upande wa pili na ndiyo yanataka kukukosanisha na ‘’mkeo’’ wa kwanza.

Nilitamani kukuambia kuwa dhumuni langu ni kukukumbusha tu kwamba umepewa jukumu na watu, fanya hiyo kazi kwa niaba ya watu na usisikilize kelele zingine.

Lakini naogopa, na nipo makini sana ninapokuambia kuwa usisikilize kelele zingine, ni muhimu ukajiuliza kuwa kwani kelele ni jambo gani?

Na kelele utaitafsilije? Na ili iwe kelele ina sifa zipi? Na je inawezekana hizo ni kelele? Au wanataka kusema kwamba unachambua kelele na kuzifanya ni sawa na sauti za nyikani? Yaani sauti za wanyonge?

Nikushauri kuwa, sasa uamue kupokea kelele za pande zote mbili, uzifanyie kazi na kuzifanya ni sauti za utulivu.

Hapa sitaki kukuchanganya, bali mwisho ni kwamba nashukuru kwa kunipa muda wa kunisikiliza, mimi pamoja na bibi, mjomba na shangazi huku nyikani hatujambo isipokuwa tunasubiri ile ahadi yako.

Ulituahidi ile ahadi yako kwenye katiba, na shangazi anakumbusha kuwa kwamba usikate tamaa maana eti, baadhi ya watu hawasahau historia.

Wanasema baadhi ya mambo yaliyojitokeza kwenye rasimu uliyoitoa hivi karibuni na tume unayoiongoza, yanafanana na uliyoyazungumza wakati ule na tume yako ileeee.

Hivyo wanahisi umehama nayo, kumbe si kweli bali haya ni mawazo ya sasa na siyo yako bali ni mawazo ya watu ingawa wakati ule na wewe ulikuwa na mawazo kama hayo na uliwahi kuyatamka.

Kwa hiyo tutafanya kila tuwezalo, kukuvalisha kaniki nyeupe ingawa mara nyingi haipatikani kwa rangi, bali kaniki nyingi zinakuwa nyeusi na zingine ni za kahawia.

Kwa hiyo piga kazi usije ukaondoka kwenye mstari, wako mpendwa kutoka huku nyikani katika maendeleo ya katiba mpya.

Nalazimika kumweleza Jaji warioba mambo haya kwasababu ameacha kushughulikia katiba ameanza kushughulika kuwajibu wanaohoji mambo ya tume kupitia vyombo vya habari.

Wenzake kwenye tume nyingi mbona walinyamaza kwenye mambo mengi? Je yeye anaguswa sana na wanaohoji kupitia vyombo vya habari?

Nimshauri kuwa aendelee na kazi yake kisha atuletee rasimu hiyo ili bunge la katiba lianze na wale waliozunguka na helkopta na wengine kwa miguu watajijua wenyewe.

Maana akiendelea kujibu kila mara, siku ya siku watu watajua kuwa ni kweli kumbe wameweka mawazo yao kwenye rasimu kuliko mawazo yetu sisi huku nyikani.

Na mimi sihitaji aanze kunijibu, maana akinijibu nitasema mengine ambapo atafikia hatua ya kuweka makarabrasha chini na kuanza kunijibu wiki nzima tofauti na hao wengine aliowajibu siku moja kisha akaomba tume iongezewe muda.

Jaji Warioba, haya ya kelele za kukubugudhi achana nayo, watu wanataka kuonekana walau wanajua ili waingizwe kwenye bunge la katiba, kwanza ni bunge la kihistoria, kwani nani hataki pesa? Utaona tu, watakao pelekwa kwenye bunge hilo wengi ni hawa unaowasikia mara kwa mara.

Hata mimi natamani niwemo, na ikiwezekana kila jimbo litoe Mbunge wa Katiba na baada ya miezi mitatu bunge linaisha watu mambo safi.

Nalisema jambo hili kwasababu hakuna mzalendo wa kweli kwa sasa, kila mtu anakuwa na malengo yake ya kiuchumi na umaarufu, hayo ndiyo malengo yaliyotujaa watanzania.

Wafanyabiashara wakubwa wanahitaji kuwa wabunge siyo kwasababu ya kwenda kuwa moja ya watunga sheria, la hasha, bali wanataka kuwa na unafuu wa manyanyaso ya mawaziri wanaoonyesha meno ya sheria kwenye biashara zao huku biashara hizo hizo zilizo chini ya wabunge wenzao hazibughudhiwi.

Watu wana malengo ya mbali kuliko wengi tunavyofikiri, wanataka kufika Ikulu ili wajenge historia au watekeleze malengo yao ambayo ni ya sirini na dhahili na wala si kuwatetea na kuwaongoza vema watanzania.

Warioba, usijali bali piga kazi, hakuna ambaye anaweza kukupindua katika nafasi uliyonayo kwasababu ina Baraka zote na Rais Jakaya Kikwete, ambaye binafsi sitaki kuamini kuwa alichokifanya kuhusu katiba eti hakijui na kufuata mkumbo.

La hasha! Bali akili yangu inaamini kuwa ambao yawezekana hawakujua walichokuwa wakikifanya bali baadhi walifuata mkumbo ni wale waliowaza kumpindua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1982, ambapo akaamua mwaka 1985 kuachia ngazi na kuanza kuongoza serikali nje ya mfumo rasmi.

Hao si wengine ni pamoja na Capt; Maganga ambaye alikuwa na umri wa miaka 26 na alishirikiana na wenzake wanane kutaka kuipindua serikali ya Mwalimu Julius Nyerere. Walikamatwa wakafunguliwa kesi ya uhaini.

Mwaka 1985 Maganga na wenzake saba; Suleiman Kamando, Zakaria Hans Pope, Vitalis Mapunda, Mbogolo, Kajaji Badru, Hatibu Gandhi (Hatty MacGhee) na Christopher Kadego walihukumiwa kufungwa maisha jela. Pius Lugangila alitoroka.

Maganga alikuwa na cheo cha kepteni ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) wakati mwenzake Mohamed Tamimu, waliyeshirikiana naye katika hatua za awali za maandalizi ya mapinduzi hayo, aliuawa na vyombo vya dola siku chache kabla ya siku ambayo walikuwa wamepanga kufanya mapinduzi hayo.

Hivyo sitaki kukukumbusha historia bali watu hawasahau historia, nawe pia endelea na majukumu wala usitujibu maana bado hatujasahau historia yako na wenzako jinsi mlivyokua mkitaka mkao serikali na ndiyo maana nawaambi watu kuwa umevaa kaniki nyeupe.

Sidhani kama nimekuchanganya katika kueleza mambo haya kwa sauti hii ya nyikani, bali ninachoamini ni kwamba ni kama unazipa uzito kelele na kuzifanya ni sauti za watu wa nyikani.

0754 440749
kalulunga2006@gmai.com
 

No comments: