Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, August 09, 2016

KESI YA MFANYABIASHARA (MFIKEMO) MBEYA YAENDELEA KUSIKILIZWA

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya

Kesi namba CC/ 94/2016 inayohusisha ndugu watano wa familia moja kumjeruhi Lwitiko Osiah Mwandemele(55)imeendelea kusikilizwa katika mahakama ya mkoa wa Mbeya baada ya upande wa mashitaka kuleta mashahidi watatu kwa ajili ya kutoa ushahidi mahakamani.

Wakili wa Serikali Gwaltu Catherine akisaidiwa na Baraka wamesema watuhumiwa wote walitenda kosa hilo juni 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika makazi ya Lwitiko Mwandemele mtaa wa vingunguti Kata ya Isyesye Jijini Mbeya.

Washitakiwa hao ni pamoja na Fredy Osiah Mwandemele(55, Alinine Osiah Mwandemele(50, Kairo Osiah Mwandemele(42),Livingstone Osiah Mwandemele(42)na Richard Osiah Mwandemele(33)ambao wote walikana mashitaka.

Walioaza kutoa ushahidi mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa Michael Mteite ni mtoto wa Lwitiko (Mfikemo )Ambilike Lwitiko akiwaongozwa na mawakili wa Serikali amesema siku ya tukio yeye alifika majira ya saa nne asubuhi katika nyumba ya baba yake inayofanyiwa ukarabati wa uzio ambapo muda mfupi alifika baba yake (Mfikemo)akiwa na gari yake.

Muda mfupi walifika Baba zake wadogo aliowatambua kwa majina Kairo Osiah Mwandemele na Richard Osiah Mwandemele wakimshambulia mbele ya mtendaji wa mtaa wa vingunguti Mariam Ngole licha ya kuwasihi waache matusi punde walifika Fredy, Alinine na Livingstone ambao walianza kumshambulia mtoto wa Mfikemo kwa mapanga , mawe na chepeo ambapo mtoto aliumizwa mkono. Hata hivyo mtendaji alimuondoa Ambilike eneo hilo lakini ndugu wote walimshambulia hadi alipoteza fahamu.

Shahidi wa pili ambaye ni Afisa mtendaji wa mtaa wa vingunguti Kata ya Isyesye Mariam Ngole ameiambia mahakama kuwa aliitwa na Richard kwenye tukio hilo ambapo anamtambua Richard kama mkazi na si mmiliki wa nyumba bali nyumba hiyo ni ya Mfikemo kutokana na nyaraka zilizopo ofisini.

Shahidi wa tatu ni fundi ujenzi Onesmo Gadau ambaye ameiambia mahakama kuwa aliwaona washitakiwa siku ya tukio ambapo walimshambulia bosi wake (Mfikemo )na mtoto wake kwa kutumia mawe, mapanga na nondo mpaka alipozidiwa ndipo walimbeba hadi kwenye gari ya Mfikemo na kukimbizwa hospitali ya rufaa.

Hata hivyo katika mahojiano kulitokea swali la kwa nini PF 3 ilitofautiana tarehe? Ambilike ameiambia mahakama kuwa aliyejaza ni Daktari hilo swali halimhusu na kwamba baadhi ya baba zake ambao ni washitakiwa hajui wanapoishi. Kesi imeahirishwa hadi Agost 17 mwaka huu upande wa mashitaka utakapoleta mashahidi wengine.

No comments: