Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, August 23, 2016

LOWASSA AKWAMA KUFANYA MKUTANO MBARALI MBEYA(Picha kwa hisani ya jf).

ALIYEKUWA mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Edward Lowassa, amekwama kuendelea na mikutano yake ya ndani aliyoianza tangu Juzi Mkoani Mbeya.

Taarifa zilizotufikia zoimeeleza kwamba, kiongozi huyo ambaye jana baada ya kumaliza mkutano wake wa ndani na wanachama wenzake wa chama hicho mjini Mbalizi Jimbo la Mbeya Vijijini, alikuwa akikusudia kwenda mkoa wa Rukwa ambako Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaendelea na ziara ya kiserikali.

Imeelezwa kwamba alipigiwa simu kwamba aahirishe ziara hiyo ambapo alitii na leo asubuhi alikusudia kufanya mkutano na wanachama wenzake Jimbo la Mbarali ambako ameshindwa kufanya baada ya kuzuiwa.

Hata hivyo kwa sasa yupo njiani kuelekea mkoani Iringa ambako taarifa ambazo www.mpakani.com zimenasa ni kwamba nako hatoweza kufanikiwa mkutano anaodhani ataufanya kutokana na sababu ambazo zinaendelea kutujia katika dawati letu la uchunguzi.

Endelea kuwa nasi.

No comments: