Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, August 31, 2016

MASWALI MAGUMU KWA WANAUME AMBAYO HAYAPASWI KUULIZWA MARA KWA MARA


KUNA maswali kadhaa mbayo wanawake hawapaswi kuyauliza mara kwa mara kwa wanaume wao, lakini utakuta bado wanawake wanakazana kuuliza mambo hayo.

Leo katika jamvi hili la mapenzinangono.blogspot.com nitajaribu kuweka wazi mambo hayo kwa ajili ya kumfunda mwanamke.

Kuna usemi unaosema kuwa, kama unataka maswali bila majibu ama majibu bila maswali zungumza na mwanamke. Ukiwa na maana kuwa eti wanawake ni moja ya viumbe wa ajabu katika dunia hii......

1. UNANIPENDA?
Jibu sahihi kwa swali hili kutoka kwa mwanaume ni ndiyo.

2.UNAFIKIRI NINI? 
Jibu analoweza kujibu mwanaume ni kumwambia mpenzi wake, ''samahani kwa ukmya, nilikuwa nafikiria ulivyo mzuri mpenzi wangu, mcheshi na mwenye fikra njema.

3. UNADHANI MWANAMKE YULE NI MREMBO KULIKO MIMI?
Neno yule, katika mapenzi, mwanamke anaweza kuwa anamaanisha mpenzi wa zamani au aliyekuwa akimtazama sana muda uliopita.

Kwa vyovyote vile, jibu sahihi ni hapana, wewe ni mzuri sana au nilikuwa nawaza mambo mengine.

4. UTAFANYA NINI MIMI NIKIFA?
Jibu sahihi ni kwamba'' maisha yatabadilika sana kwangu na kuwa mabaya na hapo nitatamani nijirushe hata kwenye gari nami nife nikufuate''

Maana mwanaume akisema kuwa ukifa ataoa mwanamke mwingine, mwanamke anaumia...

5.NIMEPOTEZA MVUTO?
Mwanaume atakujibu hapana...

Mwanamke kuwa mwangalifu kumuuliza maswali mwenza wako, mwishoni utaishia kulia.....

Endelea kupata kachumbari zenye radha mbalimbali kupitia mtandao huu kwa ajili ya elimu zaidi ya mahusiano....

No comments: