Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, August 31, 2016

MBOWE ASITISHA MAANDAMANO YA UKUTA

MWENYEKITI wa chama cha upinzani nchini Tanzania, Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe (kamanda mkuu), amewatangazia wafuasi wake wote nchini humo na kuwaambia kuwa kesho Septemba mosi, hawatatakiwa kuandamana kama chama hicho kilivyotangaza wakisubiri kupatanishwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Mbowe amesema kuwa viongozi wa dini na taasisi zingine wamewaomba kuahirisha maandamano hayo na kwamba endapo Rais Magufuli hatokubali kukaa nao mezani basi Octoba Mosi mwaka huu watafanya maandamano hayo.

Aidha amewaomba wanataaluma wakiwemo waandishi wa habari kujiunga na kile alichokiita UKUTA kwa ajili ya kufanikisha azma yao.

No comments: