Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, August 19, 2016

MKURUGENZI MBEYA ASEMA ATAWATUMBUA WATUMISHI WANAOMWANGUSHA

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ameichiory Biyengo Josephat, amesema ataanza kuwatumbua watumishi ambao wanashindwa kwenenda sawa na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.

Aliyasema hayo jana alipozungumza na mtandao huu baada ya Halmashauri hiyo kushindwa kuusafirisha mwili wa Mwalimu Steven Mvile kwa wakati, na kusababisha waombolezaji kukaa na mwili wa marehemu nje ya nyumba yake kwa zaidi ya saa sita.

Mwalimu Mvile ambaye alikuwa Mwalimu wa somo la Kiingereza katika shule ya sekondari Usongwe kisha kuhamishiwa shule ya Sekondari Ilunga zilizopo kata ya Utengule Usongwe, alifariki juzi mjini Mbalizi wilayani humo.

Baada ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya walimu waliohudhuria msiba huo kuwa mwajiri wao kawadhalilisha watumishi kwa kutotaka kuusafirisha mwili wa mwenzao, mwandishi alimpigia simu Ofisa elimu Sekondari wa wilaya hiyo, Abiud Fungamtama ambapo hakuweza kupokea simu yake.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alisema yeye alitekeleza wajibu wake kwa kusaini nyaraka alizopaswa kusaini Mara tu baada ya kupokea taarifa ya msiba huo.

"Mimi huwa sipendi mchezo kwenye kazi. Tena nilisaini document wima wima maana nilikuwa nakuja kwenye mkutano wa Arati huku Tunduma. Hao wazembe nitaanza nao maana siwezi kufanya kazi na watumishi wasioweza kuwatumikia na kutoa huduma kwa wakati kwa mwananchi" alisema Mkurugenzi huyo.

No comments: