Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, August 23, 2016

RC MAKALLA AKATAA KUGAWA ENEO LA VIWANDA KUWA MASHAMBA Umati uliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mahubiri mjini Mbalizi Mbeya Vijijini mwishoni mwa wiki, kumsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla na kutoa kero zao kwake.
 Maombi pia yalifanyika katika mkutano huo wa Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
 Aliyedhauaruliwa na wengi yeye amkumbatia na kumpa fursa ya kusema chochote mkutanoni na akampatia namba ya simu na kiasi cha fedha baada ya kumpenda kwa hoja zake.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya akiwa na baadhi ya wananchi akisalimiana nao maeneo ya Viwanja vya Mikutano Mbalizi.
Mkutano ulipoisha kwa amani na utulivu ikaanmza safari ya kuendelea na majukumu mengine.

Na Gordon Kalulunga, Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Gabriel Makala, amekataa ombi la baadhi ya wananchi waliotaka shamba mali ya kiwanda cha Nyama cha Tanganyika Packers kilichopo wilaya ya Mbeya, waliotaka shamba hilo ligawiwe kwa ajili ya kilimo cha nafaka.

Akitoa msimamo wa serikali kuhusiana na ombi hilo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo hususani katika mji mdogo wa Mbalizi, Makalla alisema kuwa Serikali ya Awamu ya tano imelenga kufufua viwanda na kujenga vipya, hivyo eneo hilo litabaki kuwa mali ya kiwanda.

“Shamba hilo litabaki kuwa mali ya serikali na ni maaluma kwa ajili ya kuchungia mifugo ambayo itakuwa inachinjwa katika kiwanda cha Tanganyika Packers na kiwanda cha Mbeya Textile nia ya serikali ni kuvifufua na kazi iliyopo ni kutafuta wawekezaji. Kufufuliwa  kwa viwanda hivyo kutaongeza ajira na masoko kwa  zao la Pamba na mifugo.” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika mkutano wake na wananchi uliofanyika katika kiwanja cha mikutano maarufu kama uwanja wa Mahubiri, alipokea kero zaidi ya 20 na kuzijibia ambazo baadhi zikihusisha tatizo la Maji,  Mgogoro wa kisiasa ndani ya Mamlaka ya mji Mdogo wa Mbalizi, mvutano wa halmashauri na wafanyabiashara wa masoko A&B , ufufuaji viwanda na ujenzi wa ofisi ya halmashauri.

Makalla aliwaonya wote wanaochochea Mgogoro wa kisiasa ndani ya mamlaka ya mji Mdogo na amemwagiza Mkuu wa wilaya hiyo William Paul Ntinika, Mkurugenzi na viongozi wa Mamlaka kukaa pamoja na kuelekezana majukumu yao, kuelewa sheria na kutekekeza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na si kwa mihemuko ya kiitikadi.

“Ndani ya wiki mbili, Mkuu wa wilaya uniletee taarifa za watu ambao hawataki kutii sheria maana wasio tii sheria mimi ndiyo wateja wangu” alisema.

Kuhusu tatizo la Maji mji wa Mbalizi amewaagiza Mamlaka ya Maji Mbeya kukaa na Mamlaka ya mji Mdogo mbalizi kuingia makubaliano ili Mamlaka ya Maji Mbeya wahudumiwe eneo la jiji na Mamlaka ya Mbalizi na kwa kufanya hivyo tatizo la Maji litakuwa limekwisha kwani Mamlaka ya Maji Mbeya wana Maji ya kutosha, watalaam, vitendea kazi vya kuboresha.

Kuhusiana  na Azma ya halmashauri kuwachukulia hatua bodaboda na  wafanyabiashara kutakiwa kuachia vyumba kama hawatalipa kiasi cha Tsh 50,000/= kutoka Tsh. 5,000/ na Tsh. 15,000/= amewagiza kukaa na kufikia muafaka ikiwemo kutoa Elimu  kwanza kabla ya kuchukua hatua.

No comments: