Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Friday, August 12, 2016

RC MAKALLA AREJESHA VIWANJA ZAIDI YA 400 KWA WANANCHI


- Ni kwa  Jiji kushindwa kulipa fidia kwa miaka 5 na mpaka sasa Fedha hazijapatikana
- Aagiza Jiji lilipe  fidia YA mapunjo kwa viwanja 603 kwa wananchi waliolipwa Fidia
- Jiji lisimamie umilikishaji  viwanja 454 kwa mujibu wa Mipango miji
- Awataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jiji na ujenzi uzingatie ramani YA Mipango miji
- Wananchi waangua vilio vya Furaha.

MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Amefanya maamuzi magumu kwa kulipoka jiji la Mbeya mpango wa kuuza viwanja 454 na kisha kuwalipa wananchi wenyeji fidia baada ya kubaini kuwa jiji kwa muda wa miaka 5 wameshindwa kuwalipa fidia wananchi hao na kuleta Kero kwa wananchi hao ikiwemo kutoyaendeleza maeneo yao kwa miaka 5 na kusababisha wananchi kuilaumu serikali.

Uamuzi huo ambao ni Faraja  kwa wananchi na mchungu  kwa jiji la Mbeya umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa katika mkutano wa hadhara mtaa wa Sisitila na kuelekeza kwa kuwa jiji lina ramani YA Mipango miji viwanja hivyo vijengwe kwa kuzingatia Mipango miji na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jiji ili wamilikishwe viwanja hivyo kisheria
Kwa wananchi ambao tayari wamelipwa fidia na kuna mapunjo ya fidia ameagiza jiji kulipa fidia  sh 798m kwa ajili ya viwanja 603.

Amewataka jiji kuachana na tabia YA kungangania  miradi YA viwanja kama jiji halina fedha badala yake katika mazingira hayo wawamilikishe wananchi viwanja kwa mujibu wa ramani ya Mipango hiyo itasaidia kuondoa malalamiko na ucheleweshaji wa fidia

No comments: