Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, August 23, 2016

SHAUNAE MILLER; MWANARIADHA ALIYEPATA MEDALI KWA KUJIANGUSHA

Shaunae Miller akiteleza wakati wa kumaliza mbio za mita 400 Olympic Rio 2016
Michuano ya olimpiki imemalizika nchini Brazil, huku ikiweka rekodi ya kuwa na matukio mbalimbali ya kuvutia na kustaajabisha.


Miongoni mwa matukio hayo ni medali ya kwanza mwaka huu nchini Bahama kupatikana kwa njia ya kujirusha kupitia kwa mwanariadha wake Shaunae Miller.

Miller alimaliza akitumia muda bora zaidi kwake msimu huu wa sekunde 49.44 akimtuma Mmarekani Allyson Felix aliyetumia sekunde 49.51 na nafasi ya tatu ikikamatwa na raia wa Jamaica akitimua vumbi kwa sekunde 49.85.
Hali ilivyokuwa
Shaunae Miller akiwa chini baada ya kumaliza mbio za mita 400 karika Rio 2016
Wakati mbio zikianza, mwanadada Miller alionekana kuwa imara na kuongoza katika mita 400, lakini alikuja kupitwa na Allyson Felix wa Marekani.
Wakati wakikaribia kumalizia mita 400 walionekana kama kuwa sawa, huku Allyson akiwa na matumaini makubwa ya kutwaa medali ya dhahabu ndipo Miller alipoteleza hivyo kuwa mbele ya Mmarekani.
Katika hatua hiyo shingo zao zilikuwa sawa huko Allyson akijielekeza zaidi kutaka medali hiyo.
Hata Mmarekani hadi dakika ya mwisho hakuwa amefahamu nani aliyeshinda mbio hizo, “Sikuwa na hakika, hapana” alinukuriwa Allyson.
Allyson alikiri kwamba mwanariadha huyo wa Bahama hakuwa kufanya kitendo kama hicho licha ya kwamba kilimuudhi sana.
Aidha mjadala mzito uliibuka katika mitandao ya kijamii kama kujirusha kama alivyofanya Miller kilikuwa kitendo kinachokubalika?
Miller alinukuriwa akisema, “Kilichokuwapo katika ufahamu wangu ilikuwa ni kutwaa medali ya dhahabu, kilichofuata nilijikuta chini, zilikuwa hisia za kustaajabisha…mpaka sasa sijajua nini kilichotokea.”

Je ushindi ni halali
Ushindi wa Miller uko sahihi kutokana na sheria kuweka wazi, “Mwanariadha wa kwanza ambaye kiungo kimojawapo kitakuwa kimetangulia (torso) na kuvuka mstari ndiye atatangazwa mshindi.”

Torso inajumuisha shingo, kichwa, mikono, miguu, viganja vya mikono na nyayo.
 
Ikumbukwe mrukaji mahiri wa vihunzi raia wa Brazil João Vitor de Oliveira alishinda mita 110 katika nusu fainali kwenye michuano hii kwa kujirusha.

Mwaka 2008 kwenye michuano ya olimpiki, Mmarekani David Neville alitwaa medali ya shaba katika mita 400 kwa kujirusha kama alifanya Miller.
Wasifu wa Sahunae Miller
Shaunae Miller akishangilia baada ya kutwaa medali ya dhahabu katika Rio 2016
Alizaliwa Aprili 15, 1994 katika mji wa Nassau nchini Bahamas, kwa sasa anaishi nchini Athens nchini Ugiriki na Georgia nchini Marekani na ana uzito wa kilogramu 69.

Mpaka sasa ametwaa medali tatu za dhahabu katika olimpiki, moja ya fedha na nyingine ni ya shaba.

Za dhahabu aliweka rekodi katika michuano ya dunia kwa vijana mwaka 2011 mjini Lille, Ufaransa.

Michuano ya Junior mwaka 2010 mjini Moncton yalimpa meda ya dhahabu.

Mwaka 2014 alishiriki katika michuano ya ndani riadha ya ndani mjini Sopot akiambulia medali ya shaba.


Pia mwaka 2015 jijini Beijing aliambulia medali ya fedha katika michuano ya riadha ya dunia.

No comments: