Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Tuesday, August 30, 2016

VIGOGO MBEYA WAGAWANA VYUMBA SOKO LA MWANJELWANa Gordon Kalulunga

BAADHI ya viongozi wa idara za serikali mkoani Mbeya, wamegawana vyumba vya soko la Mwanjelwa na kuwaacha baadhi ya wahanga ambao ndiyo walitakiwa kupewa kipaumbele cha vyumba hivyo. Imebainika.

Viongozi hao ambao majina yao yanahifadhiwa, walifanya mchezo huo ambao ni mchezo wa pili kutoka ule wa ulaji wa fedha za ujenzi wa soko hilo ambao hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amoss Makala ameubaini na hivi Katibuni Waziri Mkuu alitoa maagizo ya kufanyika uchunguzi wa fedha za ujenzi wa soko hilo.

Hivi karibuni, Mkuu huyo wa Mkoa alitoa taarifa ya maagizo ambayo alipewa na Waziri Mkuu Agosti 9, mwaka huu mjini Mbeya kuhusu suala la wahanga wa soko la Mwanjelwa na harufu ya ufisadi katika ujenzi wa soko hilo.

Makalla anasikika katika sauti aliyorekodiwa akisema kuwa, baada ya yeye kukabidhiwa ofisi ya mkoa huo tarehe 17.03.2017 alinusa harufu ya ufisadi katika soko la Mwanjelwa.

Anasema licha ya madiwani kuchaguliwa, walipaswa kufika kwa wahanga wa soko hilo ambalo liliteketea kwa moto mwaka 2006 na kuona jinsi gani wanaweza kupewa vyumba, lakini cha ajabu hawajafanya hivyo mpaka alipoenda yeye na wao kukasirika.

Soko hilo ambalo awali lilitarajiwa kujengwa kwa Bilioni 13, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa soko hilo limejengwa kwa Bilioni 26 na wananchi wa Jiji hilo kupitia kodi zao za ndani wanapaswa kuilipa benki ya CRDB Bilioni 61 ikiwa ni pamoja na Riba ya fedha ambazo Jiji lilikopa kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo.

“Baada ya kunusa harufu ya ufisadi na kuomba taarifa ya ujenzi, walinidanganya kuwa walijenga kwa Bilioni 23 na nilipoteua kamati kwa kuhusisha vyombo vya dola ikabainika kuwa soko limejengwa kwa Bilioni 26”…

“Siku niliyoenda soko la mwanjelwa, maana kuna baadhi ya viongozi wanaohusika walitoka katika kikao changu na ilikuwa meseji kuwa anayeingia anakanyaga mikono yetu” alisema Makalla.


Alisema baada ya awali kupata taarifa za Jiji hilo la Mbeya ambalo linaongozwa na Chadema, alibaini kuwa taarifa za Jiji hazikuwa sahihi na haikuzingatiwa uanzishwaji wa ujenzi wa soko lile na kwamba mhanga ndiye aliyetakiwa kupewa kipaumbele badala yake wahanga wamebaki mguu ndani na mguu nje katika eneo la Sido.
Baada ya kuchukua maamuzi ya kutembelea soko hilo na kunusa harufu ya ufisadi, anasema alidhani atapewa pongezi na hasa madiwani, lakini ndiyo walikuwa wa kwanza kutoka kwenye kikao na kukimbia.

“Sasa nataka niwahakikishie kuwa taarifa ya awali zinaonyesha kuwa kuna fedha Milioni 489 zinatoka akaunti Ya Jiji kulipwa CRDB, ndiyo maana Waziri Mkuu aliniagiza kuwa harakisha suala hili maana CRDB hazionekani na alitoa siku tatu” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Alieleza kwamba, kamati aliyoiunda baada ya agizo la Waziri Mkuu, imebaini kuwa fedha hizo zimelipwa CRDB hivyo CAG na watu wa mifumo wa Benki kuu watapiga kambi pale ili kubaini matatizo ya pale CRDB kubaini ukweli wa fedha hizo zilikoenda na kwamba ameshusha bei vyumba hivyo kutoka pango la Shilingi 500,000/= mpaka 350,000/= na 250,000/=

“Vyumba pale wamegawana viongozi na nitawataja hapo baadae. Kuna watu wana vyumba vitano wengine kumi na wiki ijayo nitakuja hapa kuwanyang’anya vyumba na kuwapa watu wengine” alisema Makala.

Kuhusu watu wanaouza bidhaa barabarani pembeni mwa soko la Mwanjelwa, amebainisha kuwa kamati yake imempa mapendekezo na kwamba ndani ya uzio wa soko hilo serikali yake itajenga vibanda vidogovidogo vipatavyo 140 ambavyo vitatumiwa na wamachinga hao.
Apeleka njaa kwa madiwani

“Nimepiga marufuku madiwani kusafiri na kupewa posho na mafuta kupitia timu ya Mbeya City. Huo utaratibu ni marufuku. hawatosafiri ni maamuzi yasiyo na tija na ni bora maana wao siyo makocha na pesa hizo bora wapewe wachezaji kama motisha. Nimeanza kazi sijaribiwi na sirudi nyuma”.

“Mambo ya soko la Mwanjelwa, kama kuna watu wanaona kuna urasimu wa kupewa vyumba nataka majina. Kamati imeshachunguza na wamenipa taarifa na ninajua chumba gani na wiki ijayo naenda kuwatoa wote” alimaliza Makala.

Mwisho.

No comments: