Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Sunday, August 28, 2016

WANANCHI MLOWO SONGWE WAINGIA MGOGORO NA POLISI

Hali ya uvunjifu wa amani umejitokeza Mji mdogo wa Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe baada ya wananchi kuchoma moto barabarani kwa magurudumu ya magari barabara Kuu ya TANZAM Mbeya /Tunduma.

 Tukio hilo limetokea majira ya mchana Agost 28 mwaka huu baada ya wananchi wa Mlowo kudai kuwa mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Stanslaus Kalinga (42) kudaiwa kupigwa na Askari baada kukamatwa kwa kosa la uzembe na uzururaji. Marehemu amefia hospitali ya Wilaya ya Mbozi akipatiwa matibabu.

Diwani wa Kata ya Mlowo Sebastian Kilindu amekiri kutokea kwa tukio hilo na baadaye alikwenda Polisi ili kupata ukweli wa tukio hilo .

 Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Mathias Nyange amesema kuwa Jeshi la Polisi lilimkamata marehemu na hakupigwa na Polisi kama inavyodaiwa kwani taarifa kamili juu ya kifo hicho ataitoa baada ya uchunguzi wa Daktari.

Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa Mlowo walibeba chakula kutoka msibani na kupeleka kituo cha Polisi Mlowo kwa kile walichodai kifo cha marehemu kimesababishwa na Askari hivyo nao washiriki kula.

Hali hiyo ilisababisha polisi kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya  wananchi hao . Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mlowo alimuomba Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe kufanya suluhu na wananchi hao kwa kuwa Askari hawana kambi wanaishi nao mitaani hivyo mgogoro huo utatuliwe kwa amani .

Hata hivyo bado hali imekuwa tete kutokana na wananchi kughadhabika licha ya kwamba vurumai zimetulizwa.

No comments: