Social Icons

ad3

ad3

ad2

ad2

ad1

ad1

Wednesday, September 28, 2016

Dawa za kulevya aina ya Cocaine


Na Gordon Kalulunga-Tanzania

Makundi rika na kuiga ni moja ya sababu inayopelekea baadhi ya vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo Bangi, Mirungi, Cocaine, Petrol na vileo mbalimbali.

Leo naangazia dawa za kulevya aina ya Cocaine ambayo inatengenezwa na mmea uitwao Coca ambao unastawishwa katika nchi za America ya kusini.

Dawa hii ipo katika kundi la kichangamshi kikali ambacho huathiri mfumo wa fahamu.

Cocaine huwa katika unga mweupe au katika hali ya mawe madogo madogo.

Majina ya mtaani huitwa unga. White suger, keki, big c, bazooka, snow na unga mweupe.

Kinachotokea baada ya kutumia Cocaine, mtumiaji huchangamka kupita kiasi, kupungua kwa mboni za macho, kupungua kwa hamu ya kula, kukauka koo, kutokutulia, kuwa na mhemko wa kufanya ngono, kusinyaa kwa mishipa ya damu, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

Madhara kwa mtumiaji ni kuwa na maono au njozi zisizo za kweli, kuchanganyikiwa, kuwashwa mwilini, kuwa na hasira za ghafla, hisia za uwepo wa vijidudu mwilini, kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo kunakoweza kusababisha kiharusi au kifo, kuongezeka na kupungua kea mapigo ya Moyo ghafla, kutetemeka kwa nguvu kama kifafa, utegemezi, kuvunja Sheria na matatizo ya kisaikolojia.

Uwepo wa mwathirika mmoja, jamii nzima inaathirika.

Kutumia dawa za kulevya kunachochea zaidi kupata magonjwa yatokanayo na ngono ukiwemo Ukimwi.

Tuungane kutoa elimu na kupinga matumizi ya dawa za kulevya nchini ili jamii yetu iwe salama.

No comments: